MAMA GETRUDE MONGELA AGUSWA NA ACT-WAZALENDO AIBUKA NA KUIMWAGIA SIFA KIBAO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Bi Getrude Mongela akizunguza na waandishi waHabari leo jijini Dar es Salaam |
ALIYEKUWA
Spika wa Bunge la Afrika ambaye pia ni Mwanaharakati wa Wanawake nchini Bi Getrude Mongela ameibuka na kukipongeza chama
cha ACT-Wazalendo pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM kwa hatua walizofanya za
kumteua mwanamke katika hatua za nafasi za juu za Urais.Aaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari
leo Jijini Dar es Salaam Bi Mongela amesema vyama hivyo vinafaa kupongezwa kwa
kuonyesha kumjali mwanamke ikiwemo katika kumteua mwanamke natika nafasi ya
uongozi akidai yote imetokana na mpango kazi wa Bejing (Bejinng platform of
action)ambao ulilenga kumwinua mwanamke.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Bi Mongela |
Amesema hatua ya ACT-Wazalendo kumteua Mwanamke
ambaye ni Anna Mghwira kuwa Mgombea Urais
wa chama hicho,na chama cha CCM kumtea mama Samia Salum kuwa makamu wa Urais wa
mgombea wa Urais wa chama hicho kwa kudai hayo yote yameleta mapinduzi makubwa
katika harakati za kumuinua mwanamke
nchini.
Bi Mongela ambaye alikuwa Katibu
mkuu wa uliokuwa mkutano uliojulikana ni wa Beijing ambao uliitishwa kwa lengo
la kumuinua mwanamke dunia ambapo amesema katika miongoni mwa malengo ya
mkutano huo ulikuwa na moja ya ajenda ya mwanamke kupatiwa nafasi za juu za
kugombani nafasi za uongozi,lakini kwa hatua iliyotokea nchini amezidi dai ni
ishara ya mapinduzi makubwa kwa wanawake nchini.
pichani ni Mkurugenzi wa TNGP Bi Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari |
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa
Kijinsia nchini TNGP Bi Lilian Liund amesema kwa sasa umoja huo hautakubali
kukiunga chama chochote cha siasa ambacho hakitampa mwanamke nafasi za juu
ikiwemo, Urais,makumu wa Rais pamoja Uwaziri mkuu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni