Zinazobamba

JWTZ LAMJIBU LOWASSA,LAIBUKA NA KUSEMA MANENO HAYA,SOMA HAPO KUJUA





Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akikanusha jeshi hilo kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa. Kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omari.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mgombea wa Urais kupitia Cha cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Edward Lowassa  na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na  kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.

"Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa.

Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.

Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo.

"Wananchi na viongozi wa kisiasa mnaombwa mfanye kazi zenu za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa wananchi" alisema Kanali Lubinga.

Kanali Lubinga alisema jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani wananchi wanaimani na jeshi lao.
kuibuka huko kwa JWTZ kunakuja ikiwa imepita siku chache baada ya lowassa kuibua tuhuma kwamba na kuna watu wanapita kwa wanajeshi la kuchukua namba za kadi ya kupiga kura na kumuagiza Kiongozi wa Chadema Mabere Marandu kufuatilia hali hiyo 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Maoni 4

Unknown alisema ...
Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
Bila jina alisema ...

je wanayo haki ya KUPIGA KURA ?
KAMA WALIVYO WATANZANIA WENGINE ?

afkombo alisema ...

Ndiyo. Kula Mwanajeshi Ana haki ya kuchagua kingozi anayemtaka. Anachokatazwa Mwanajeshi Ni kushabikia Chama cha siasa.

Unknown alisema ...

You have authority to do so
Unless otherwise