HABARI KUBWA LEO-LOWASSA AIPA MAJANGA ITV,TCRA YAILIMA,SOMA HAPO KUJUA
EDWARD
Lowassa ni kama ameanza kuipa majanga kituo cha Televisheni Cha ITV ndivyo
naweza kusema baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kukitaka kituo
hicho kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari pamoja
na kupewa onyo kali baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es
Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya
Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi
(pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Muyangi amsema kamati hiyo imebaini kituo cha ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini
kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.
Amedai katika kipindi cha Habari zilizotufikia mda huu kilichorushwa
siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi ambapo
katika kipindi hicho kilirusha taarifa kuhusu “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais.
Amesema katika kipindi hicho
Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya
kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndipo amesema hivyo,Wakati
taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo alikuwa alijasema taarifa
hizo..
Be Muyangi amesema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya
kwanza juu kuzuiliwa huko kwa maandamano,
ndipo siku hiyo hiyo tena katika kipindi
hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa
taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao
makuu wa Chama chaWananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC amedai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya
Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza
haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.
Amesema Baada ya Mamlaka hiyo
kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa Itv Be Mhavile na
mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa.
Ili kutaka ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikili kosa
hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii
ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa kuithibitisha kama taarifa hiyo kama ni ya
kweli au la.
Aidha, Be Muyangi amesema baada ya Kamati
hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya
Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha
taarifa zinatazoleta mchanganyiko katika jamii,
Ndipo
wakatoa hukumu ya kuitaka ITV kuomba radhi
mara mbili kwenye taarifa za habari ya asubuhi na jioni kwaanzia hukumu hiyo
ilipotolewa leo na kupewa onyo kali.
Maoni 1
How about updates
Chapisha Maoni