HABARI KUBWA LEO,CHADEMA YAMUANGUKIA ASKOFU PENGO,NI KUHUSU DOKTA SLAA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Dokta Slaa |
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemuangukia Askofu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama POLYICARP Kardinali PENGO ili kumsihi Katibu mkuu wa Chama
hicho Dokta Wilbroad Slaa abadili uamuzi wake wa kujuzulu kisiasa.(Mtandao huu umedokezwa)Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo .
Dokta Slaa
ambaye imetajwa kufikia umaamuzi wa kuachana na siasa baada ya kutorizishwa na
chama chake kuhusu uamuzi wa kumchukua Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na kumpa nafasi ya kuwania Urais.
Taarifa za
kuaminika toka ndani ya Chama cha Chadema zinasema kwa sasa chama hicho ni kama “kinahaha”
kutafuta kile kinachotajwa kila aina ya njia kumzuia Dokta Slaa asifikia
umamuzi huo, kwa madai ya kukiacha chama hicho sehemu mbaya.
Mtoa taarifa
wetu huyo wa Fullhabari.blogs, amesema kwa sasa chadema kimeanza hata kuwatumia
viongozi wa kiroho akiwemo Askofu pengo, kwa madai ya kuwa na ushawishi mkubwa
kwa Kiongozi huyo wa Chadema.
“Yaani sahivi
ujuo wa lowassa,sasa ni kama umekuwa mwiba ndani ya chama chetu,hatua anayotaka
kuchuka Slaa ni mbaya sana,na ndio maana viongozi wetu,usiku na mchana
wanahangaika kumturiza asifanye hivyo na ndio maana wameamua hadi kumia Askofu
Pengo kuokoa Jahazi”kimesema chanzo chetu hicho kwa sharti la kutotaja jina
lake.
Pichani nia Askofu Pengo |
Ameongeza kuwa “Ujue Slaa na Askofu Pengo ni
marafiki sana hata kipindi kile cha nyuma alipokuwa “mtawa” kwahiyo chama
kimeona kumtumia kiongozi huyu wa kiroho kunaweza kukisaidia chama chetu kumbadili
Slaa na umuzi wake wa kustaafu siasa,maana bila Slaa chadema ni kazi bure”
Kuibuka kwa
taarifa hizi,kuna kuja ikiwa ni siku chache baada ya Gazeti moja la kila siku
kuripoti kuwa Dakta Slaa ameachana na siasa baada ya madai ya kutokubaliana na
chama chake kumchukua Lowassa mbaye mara zote Lowassa alipokuwa CCM,Slaa
amekuwa akimnadi ni Fisadi.
Alipotafutwa na Dakta Slaa na Chanzo cha
Mtandao huu,ambapo alisema kuwa taarifa za yeye kuachana na siasa ni za uongo
na kudai yeye yupo chadema,
Na akaenda mbali
kwa kusema kutokuwepo ndani ya Ofisi ya
Chadema sio kwamba amekihama chama chake.
UTATA WA DAKTA SLAA
NA CHADEMA.
Utata huo
alianzia mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kikao kilichoandaliwa na Vyama
vya Upinzani vinavyounda Umoja wa kutetea Katiba ya wananchi Ukawa wakati
wakimkabidhi Lowassa kadi ya Chadema,ambapo Mkutano huo ulihudhuliwa na
viongozi wote wa Chadema pasipokuwepo na Dakta Slaa,
Sanjari pia,
utata ulizidi kuwepo baada ya Jana Lowassa alipojitokeza Makao mkuu ya Chadema wakati wa kuchukua fomu
ya Urais ambapo katika ofisi hiyo iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam pia
Katibu huyo hakuwepo Ofisini hapo Jambo ambalo linazidisha shaka.
WADAU MBALI MBALI WANENA.
Akizungumza na Fullhabari.blogs mwandishi mwandamizi wa Gazeti
la Imman ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni Beta Media ambayo ndio inamiliki
mtandao wa Fullhabari,Bwana Suleiman Magari amesema anachofanya Dakta Slaa ni
mfumo wa kidhehebu uliopo nchini.
“Ujue
hapa tunapepeza macho bure tusema ukweli,ujua hapa nchini tangu taifa hili
lipate uhuru,kwenye nafasi ya Urais pindi akisimama Mgombea wa Urais kwa upande
wa dini ya kikristo lazima awe dhehebu la Mkatoriki na huyo Lowassa ni Mluteri
ndio maana Dakta Slaa wanagoma kumuunga mkono huyo hapo kuna utata”amesema
Magari
Hakuna maoni
Chapisha Maoni