Zinazobamba

BREAKING NEWS,LOWASSA AICHANGANYA CCM,WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI NUSURA WAZICHAPE NA GADAFI,SOMA HAPO KUJUA

pichani ni Katibu Mwenezi Mkoa wa Dar es SalaaJuma Gadafi akizungumza na waandishi Habari mda huu ,

CHAMA cha Mapinduzi CCM ni kama kimeanza kupagawa ndivyo naweza kusema baada ya kushindwa kujibu tuhuma zilizotolewa na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa alizozitoa kwa chama hicho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
                Hali hiyo imejitokeza mda huu Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano uliohitishwa na chama hicho ili kujibu tuhuma alizozitoa Lowassa ambaye amekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa kusema chama chake kimekiuaka misingi ya haki katika "kuchuja" majina ya wagombea wa Urais.
                 Katika  hali isiyotegemea na wengi waandishi wa Habari pamoja na Wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari walitokeza kwenye Hoteli moja hapa jijini huku mkutano huo ukirushwa (live) yaani moja kwa moja na kituo cha Azam TV, ili kusikiliza wito ulitolewa na chama hicho .
        Ambapo taarifa za awali zilisema kutakuwa na mkutano na waandishi wa Habari ambapo mzungumzaji atakuwa Katibu Mwenezi wa Itikiadi wa CCM Nape Nnauye,licha ya taarifa hiyo kusema hivyo, la kushangaza mapaka saa saba mchana kufika waandishi wa habari walikuwa kwenye mkutano hao huku wakijua anakuja Nnauye.
        Tofauti na matarajiao hayo ilishangazwa mzungumzaji alikuja  kwenye mkutano huo alikuwa Katibu wa Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Juma Gadafi,jambo ambalo lililowakela waandishi na wahariri.
        Wahariri hao walichukia kitendo hicho wakisema kwamba Lowassa alisema mambo mazito tena yanahusu viongozi wa juu wa chama na hata Rais wa nchi,inakuwaje chama hicho kinamtume mtu ambaye hana ujumbe kwenye Kamati kuu CC na Ujumbe wa Mkutano wa halmashauri kuu NEC.
             “Ujue ccm wasitufanye sisi waandishi ni wajinga wametuletea mtu gani huyu,hivi huyu anawezaje kujibu tuhuma kama zile alizotoa lowasa huyu hana ujumbe wa NEC na CC inakuwaje haje kujibu mambo mazito”amesema Bwana balile ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Jamuhuri.
         Naye Mhariri wa gazeti La Tanzania Daima Martin Marela alisikia akisema siku nyengine waandishi wa habari watagomea mkutano wa CCM.
   
   Maneno hayo ndiyo yakamfanya Gadafi kusema
            “maneno aliyoyasema Lowassa aliyatoa ndani ya mkoa Dar es Salaam ni vema jambo hilo wakusemea ni sisi viongozi wa Mkoa”
     Huku waandishi wakimzomea Gaddafi. 
            Akijibu tuhuma za Lowassa,Gaddafi amesema kuhama kwa lowassa hakuwezi kukuathiri chama hicho kwa kudai kuwa wameondoka wanachama wengi na chama hicho bado kikazidi kuwa madarakani.

            “Tuhuma alizotoa ni za kitoto na siwezi kukujibu,ila chama chetu hakiwezi kufa nawahakikishia,maana walikuewepo wakina mrema na wameondoka je chama chetu kimepotea si bado kipo madarakani,ndio maana nawaambieni CCM inakwenda kushinda uchaguzi mkuu,”asema Gadafi

Hakuna maoni