WAZIRI LUKUVI AKUBALI KUWEPO WEZI WIZARANI KWAKE,NI WALE WANAOWAHUJUMU WANANCHI,SOMA HAPA KUJUA

WAZIRI wa
Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(pichani) amekili wizara yake
imegubikwa na rushwa kubwa kwa Watendaji wa Ardhi Jambao ambalo anasema
limeleta uhasama kwa wananchi na kuzidisha migogoro ya Ardhi nchini.Anaandika
KAROLI VINSENT,endelea nayo
Waziri Lukuvi amesema hayo leo wakati
wa Mkutano uliowakutani watumishi wa Sekta Ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam wenye
lengo la kuwapa uwezo ili wafanye kazi bila kuwepo kwa kero kwa wananchi ambapo
Waziri lukuvi amesema kwa sasa hali ya migorogoro ya Ardhi ndani ya mkoa wa Dar
es Salaam imekuwa kubwa sana inaimesababishwa
na utendaji mbovu jambo ambalo
anasema limewafanya wananchi wakose na Imani na Serikali.
Waziri Lukuvi ameongeza kuwa
hata jambo la kuchelewesha kutolewa kwa hati za Viwanja kwa Wananchi limesabishwa
na watendaji hao kuzidisha Urasimu wa kutoa Rushwa kwani amesema kwasasa
wananchi wamekuwa wakisota kwenye Halmashauri mbalimbali kutaka kupata hati ya
viwanja kwa mda wa miaka 15.
Amebainisha kuwa Suala la Hati ya
viwanja kisheria linatakiwa kumalizwa ndani ya miezi sita na Mwananchi
kukabidhiwa hati yake,lakini kutokana na Utendaji Mbovu wa watendaji umechangia
hati hizo kucheleweshwa kwa wananchi.
Aidha, Waziri Lukuvi amesema kama
kiongozi safi hato kubali kuona urasimu na akawataka watendaji ndani ya siku 20
wawe wametatua tatizo la mgogoro wa Ardhi.
Vilevile Waziri Lukuvi Akawataka
Wananchi kutosita kutoa taarifa kwenye Viongozi husika kwenye Wizara hiyo ili
hatua zishukue kwa Watendaji ambao anasema ni kikwazo kwenye wizara yake
No comments
Post a Comment