Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-MBOWE AUMBULIWA NA NEC,KAULI YAKE YASUTWA,SOMA HAPA KUJUA



TUME  ya uchaguzi nchini (NEC)imesema tarehe ya Uchaguzi mkuu Mwaka huu,ipo pale pale siku ya terehe 25 mwezi octoba mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
    Kauli ya NEC inakuja ikiwa siku moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe kuitangazi serikali kiama endapo itasogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu kwa –
Madai ya tume hiyo kushindwa kuwaandikisha wananchi kwa wakati kwenye Daftrari la wapiga kura kwa mfumo mpya wa Biometric Vote Regislation BVR.
         Akifanunua Kauli hiyo ya Mbowe mda huu Jijini Dar es Salaam naMwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema taarifa zinazosemwa na wanasiasa kwamba tume hiyo itasogeza mbele uchaguzi Mkuu  si za kweli zinalengo la kuwachanganya wananchi,kwani tume hiyo inakwenda vizuri na uandikishaji wa Mfumo mpya wa BVR.
       Jaji Damian ameongeza kuwa kwa sasa Uandikishaji wa Wapiga kura kwenye Mkoa wa mdogo wa Njombe wanatarajia kumaliza kesho na kuanza rasmi uandikishaji kwenye mikoa mingine ya Mtwala.lindi na Iringa ambapo anasema kwa sasa watafanya kwa kasi zaidi.
         Amebainisha kuwa tatizo la lilokuwa linawakabili kwa kuwa na mashine chache za uandikishaji wameliweza kulitatua kwakuwa sahivi tayari mashine zengine 1600 zinatarajiwa kuwasili siku ya kesho na kuongeza idadi ya mashine za sasa 250 jambo ambalo anadai litafanikishwa kasi ya uandikishaji.
         Aidha,Amesema shehena nyingine ya mashine itarajiwa kuja tarehe 25 mwezi huu na mpaka ifikapo mwezi wa Sita mwaka huu watakuwa wameshapata mashine zote elfu nane walizokuwa wakiziitaji jambo ambalo anazidi dai litawafanya wamalize kuwaandisha wananchi nchi nzima kwenye mwezi wa saba mwaka huu.

       Vilevile Jaji Damian akawataka wanasiasa kuwacha kuwapotosha wananchi kuhusu uandikishaji huo jambo ambalo anasema linaweza kuleta machafuko nchini.

No comments