Zinazobamba

BREAKING NEWS-NYUMBA YA ASKOFU GWAJIMA YAZINGILWA KUNDI LA POLISI SOMA HAPA KUJUA


HABARI zilizotufikia mda huu zinasema nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josepht Gwajima (pichani) imezingilwa na kundi la Polisi, kwaanzia Majira ya saa moja asubuhi ya leo, huku Askofu huyo akijifungia ndani ya nyumba yake akikataa kufungua mlango.
        Kwa mujibu wa Mwandishi wa Mtandao huu KAROLI VINSENT aliyoko Nyumbani kwake Askofu Maeno ya Tegeta Jijini Dar es Salaam zinasema Zaidi ya magari manne ya Polisi aina ya Difenda zimezingila nyumba hiyo wakiwa na lengo la kumsubili kiongozi huyo wa kiroho atoke ili wamtia nguvuni pamoja na kufanya msako kwenye nyumba yake.
Mtandao huu ulimtafuta Kamanda kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kutaka kujua kurikoni wamenda gafla kwenye nyumba ya Askofu huyo haya ndio majjibu yake aliyomjibu Mwandishi wetu.
“Acheni mambo yenu ya kiundishi wa Habari hapa nipo kwenye Kikao muhimu sana hayo ya Askofu Gwajima nitawajibu baadae”amesema Kamishna Kova

ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU UTAPATA TAARIFA KAMILI BAADAE

No comments