WANAFUNZI CHUO CHA SAUTI WAMUANGUKIA LOWASSA,WAUNGANA NA WENZAO KUMPIGANIA SOMA HAPA KUJUA
Shinikizo
la kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuchukua fomu ya kugombea
urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu, limeendelea na safari hii
wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya jijini Mwanza, wakitoa tamko la kumtaka
kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Wakizungumza na waandishi wa
habari jana jijini hapa, viongozi wa vyuo vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino
(SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi
na Tiba za Afya (CUHAS), walimtaka Lowassa kuchukua fomu ya kuwania urais
wakati ukifika.
Viongozi hao waliyazungumza hayo
wakati wakikabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto yatima
cha Upendo Daima, jijini Mwanza.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa
CUHAS, Godfrey Kisigo, alisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa sababu
anapendwa na kila Mtanzania.
Alisema wanamuomba muda
ukifika awe mtu wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi ya
urais.
“Tamko hili ni la vyuo vikuu vyote
vya Mwanza, sauti zetu ni za busara kwa sababu zinataka kuikomboa nchi yetu kwa
miaka 10 ijayo, tunayo imani kubwa na Lowassa katika hatma ya nchi hususan
elimu kwa watu wote,” alisema na kuongeza:
“Hatma ya nchi hii ipo mikononi mwako
na sisi wanavyuo hatuwezi kusubiri kuona tunakosa kiongozi atakayelisaidia
Taifa kwa kuzibwa midomo, tupo tayari kufa ili uwe rais uokoe watakaobaki na
Tanzania.”
Waziri Mkuu wa Serikali ya
wanafunzi SAUT, Christopher Mkodo, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisijaribu
kukata jina la Lowassa kwani Tanzania bila kiongozi huyo Watanzania watakuwa wamenyimwa
fursa ya kupata maendeleo ndani ya miaka 10.
Waliitaka CCM kusikiliza maoni ya
wanachama wake vinginevyo chama kitaharibika.
Mwakilishi wa CBE, Paul Dotto, alisema
Lowassa ni chaguo la wanafunzi wa vyuo vikuu na wana imani ataifikisha Tanzania
katika uchumi wa kati kabla ya malengo yaliyowekwa na Serikali.
No comments
Post a Comment