DC MAKONDA HANA USAFI WA KUMTUHUMU GWAJIMA,SOMA HAPA KUJUA
ANAYEITWA mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ameelekeza
asichokiamini na; anataka kutenda asichokuwa na mamlaka ya kukitekeleza. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
Amesema amemuita ofisi kwake Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ili kuelezamaana
ya matamshi yake
dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo.
Makonda amejigamba kuwa
Gwajima anatakiwa “kueleza maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba
(ya Jamhuri ya Muungano), usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo.”
Amesema, yeye ndiye mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Ameagiza jeshi la polisi
kumkamata Askofu Gwajima ili ahojiwe. Baadaye wamfikishe kwake “ili aeleze
maana ya kile alichokieleza.”
Ndani ya ofisi ya Makonda,
kiongozi huyo wa kidini anatakiwa kuhojiwa na “jopo la watu 20.”
Ndivyo vyombo vya habari – radio,
magazeti, televisheni na mitandao ya kijamii – vilivyomnukuu mkuu wa wilaya ya
Kinondoni.
Askofu Gwajima amenukuliwa akimtuhumu
Kardinali Pengo kwa madai kuwa amewasaliti wa viongozi wenzake wa Kikristo kwa
hatua yake ya kupinga waraka wa maaskofu kuhusu Katiba Pendekezwa na Mahakama
ya Kadhi.
Hakuna asiyemfahamu Makonda – mkuu
mpya wa wilaya ya Kinondoni. Hakuna! Vitendo vyake; kauli zake na minendo yake,
vinafahamika. Hana mamlaka ya kimaadili wala kisheria wa kusimamia anachokieleza.
Rekodi zake zipo na
zinajulikana na wengi.
Kwanza, angalau Askofu Gwajima amesema, hatapoteza
muda kwenda kumuona Makonda. Barua aliyoipata kutoka katika ofisi yake,
hataijibu. Ni barua iliyomfedhehesha; itajibiwa na maombi ya mnyororo
yanayoendelea.
Makonda hana mamlaka ya kisheria wala
kimaadili ya kumuita Askofu Gwajima.Kama kuna kesi ya jinai, wanaopaswa
kuchunguza na kushitaki, ni polisi. Siyo Makonda.
Lakini jambo ambalo liko wazi, ni
kuwa ukipitia kauli za Askofu Gwajima dhidi ya Kardinali Pengo, unagundua kuwa
alichokitenda ni madai. Siyo jinai; anayepaswa kushitaki au kulalamika katika
kaei ya madai, ni Kardinali Pengo. Siyo Makonda, wala Sulemain Kova.
Pili, ni Makonda huyuhuyu, aliyeasisi vurugu,
kulipa vijana, kuwaongoza na kisha kushambulia; naye kukiri kumpiga aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Makonda alifanya vurugu hizo
katika mdahalo ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), tarehe 2
Novemba 2014. Ulifanyika
katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Ilikuwa katikati ya mjadala, ambako
Jaji Warioba, kwa ustadi mkubwa alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine,
juu ya maudhui na kilichomo katika Rasimu ya Pili ya Katiba, ambayo ilikuwa
imesheheni maoni ya wananchi.
Mbali na vurugu za Makonda kuvunja
mdahalo, lakini pia Jaji Warioba – waziri mkuu na makamu wa Rais mstaafu wa
Jamhuri – alipigwa na Makonda na wafuasi wake. Karibu wote waliompiga na
kumfanyia vurugu Jaji Warioba, ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati Makonda anapanga
kumshambulia Jaji Warioba, alikuwa anajua kuwa alikuwa anavunja Katiba ya
Jamhuri ya Muungano, inayoruhusu uhuru wa kutoa maoni na kukusanyika.
Aidha, katiba hiyohiyo inatoa uhuru
wa Kardinali Pengo kutoa maoni yake kuhusu msimamo wa makanisa; sawa na Gwajima
alivyotoa maoni yake kuhusu Kardinali Pengo.
Lakini hata kama Gwajima angekuwa na
makosa, Makonda hana mamlaka ya kimaadili wala kisheria ya kusikiliza kesi
dhidi ya kiongozi huyo wa kiroho.
Si hivyo tu: Ni Makonda
aliyekuwa akiporomosha mvua ya matusi dhidi ya Edward Lowassa na baadhi ya
viongozi wa madhehebu ya kidini. Amekuwa akimgombanisha Lowassa na Rais Jakaya
Kikwete; Lowassa na chama chake na Lowassa na vyombo vya habari.
Hakuwahi kuhojiwa na jeshi la
polisi wala kinachoitwa, “Kamati ya ulinzi na usalama.” Bila shaka alikuwa
kazini. Alikuwa anawatumikia waliomtuma.
Hata hivyo, kesi ya Askofu
Gwajima, imerejea yaleyale ambayo yamekuwa yakielezwa kwa zaidi ya miaka 15
sasa; hakuna usawa katika taifa. Kumesheheni ukaburu.
Kuna orodha ndefu ya watu
wakikashifu mtu mwingine, wanapongezwa
kwa kupewa vyeo. Lakini wengine wanatafutwa kwa marungu, kuzuiliwa
na kufunguliwa mashitaka.
Chanzo ni mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment