MAPYAA-UTAFITI WA LOWASSA MATATANI,MWANAE ATAJWA KUUTENGENEZA SOMA HAPA KUJUA
UTAFITI uliofanywa na taasisi isiyo ya
kiserikali ya Positive Thinkers Tanzania (PTT), umeelezwa “kupikwa” kwa na
lengo la kumpendelea Edward Lowassa- Mbunge wa Monduli. Anaandika Pendo Omary …..
(endelea).
Mtoa taarifa wa chanzo changu amesema
“Kuna kila dalili kuwa, Lowassa amefadhili utafiti huu na matokeo yake ni ya
kupikwa”.
“Hii kampuni inayodaiwa
kufanya utafiti iko mtaa mmoja, jengo moja na ghorofa moja na kampuni binafsi
za Lowassa. Bila shaka ni watu wanaojuana,”amesema mtoa taarifa.
Baadhi ya kampuni
binafsi za Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu na kujiuzulu kwa kashfa ya
ufisadi wa Richmond, zinazosimamiwa na mtoto wake, Frederick Lowasa ni;
Alphatel, Barare Limited na Intergraded Property Investment Limited.
Anuani ya ofsi hizi
ni: Ghorofa ya nne, Jengo la Mavuno, mtaa wa Maktaba, jijini Dar es Salaam.
Chanzo changu kilimtafuta
Tibatizibwa Gulayi Yabatinga- Rais wa PTT, ili kujibu madai hayo ambapo
amesema, “sio kweli kwamba tumepika matokeo ili kumpendelea Lowassa”.
“Mtu yoyote kama
Bernard Membe, January Makamba na Samuel Sitta wanaweza kudhani tumeyapika.
Mbona maeneo kama Mbeya, Iringa na Mwanza ameongoza Dk. Wilbrod Slaa,” amesema
Yabatinga.
Yabatinga amesema
utafiti huo ulifanywa kwa njia ya ana kwa ana na kwa simu huku washiriki wa
njia ya simu wakipatikana kupitia mtandao wa “Whatsapp”.
“Mimi nimejiunga na Whatsapp. Nimejiunga na makundi kama sita
kwenye mtando huu. Nilichukua namba kwenye magroup (makundi), na kuwauliza
mahali walipo na nilipojua kama wapo kwenye mikoa tuliyokuwa tunafanya utafiti,
nikawahoji,” amefafanua Yabatinga.
Yabatinga alitoa majibu
hayo baada Chanzo changu kumuuliza ni namna gani waliwapata washiriki kwa njia
ya simu na namna gani waliweza kudhibiti udanganyifu wa mshiriki kuhusu eneo
analoishi.
Matokeo ya utafiti huo
yalitangazwa Jumapili iliyopita, yakionesha Lowassa akikubalika zaidi
miongoni mwa wanasiasa 15 wanaotajwa kuwania urais katika uchaguzi mkuuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Aidha, Dk. Slaa – Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anashika nafasi ya pili
akifuatiwa na Mwigulu Nchema- Naibu Waziri wa Fedha.
Utafiti huo ulifanyika Februari mwaka huu na ulihusisha mikoa 13
na kushirikisha watu 3,298.
Matokeo ya utafiti huo unaonesha CCM imeongoza kwa kupata kura
1,144 sawa na asilimia 34.68, Chadema kura 1,117 (asilimia 33.86), Chama cha
Wananchi CUF kura 360 (asilimia 10.91) na NCCR Mageuzi kura 77 (asilimia 2.33).
Washiriki katika
utafiti huo walitaja kiongozi wanayemtaka lazima awe na sifa za utendaji kwa
vitendo, uadilifu, uzoefu na elimu bora.
Wanasiasa wengine
waliopigiwa kura ni; Prof. Ibrahimu Lipumba, John Magufuli, Zitto Kabwe,
Bernard Membe, Mizengo Pinda, January Makamba, Prof. Mark Mwandosya, James
Mbatia, Dk. Hussein Mwinyi, Steven Wasira, Fredrick Sumaye na Samuel Sitta.
Chanzo Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment