TGP WAMUANGUKIA RAIS KIKWETE,NI KUHUSU MSWAADA WA MTANDAONI SOMA HAPA KUJUA
| pichani ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa TGP Bwana Temba Akitoa semina ya mafunzo kwa waaandishi na Wamiliki wa Blogs mbalimbali |
WADAU mbali
mbali wameendelea kumlilia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Rais Jakaya
Kikwete asisaini Maswaada wa sheria ya uharifu Mitandaoni wa mwaka 2015 kwa
kusema mswaada huo unavingere ambayo
wanasema vitauzikia Uhuru wa Habari
nchini na pamoja na uhuru wa kutoa maoni
kwa wananchi.Anaandika KAROLI VINSENT.Endelea nayo
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao
wa Jinsia nchini (TGP) Lilian Liundi wakati wa Semina iliyowakutanisha waandishi
mbalimbali na wamiliki wa Mitandao ya Kijamii yenye lengo la kuwajengea uwezo
wa kuripoti taarifa mbalimbali hususani katika kipindi hiki muhimu cha kura ya
Maoni ya kupitisha katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba pamoja na Uchaguzi Mkuu
hapo baadae Mwaka huu.
| Waaandishi Mbali mbali wa Mitandaoni wakiwa kwenye makini wakisikiliza mafunzo yanayotolewa na Watendaji wa TGNP |
Ambapo Bi Liundi amesema licha ya
mswaada huo kuwa na vipengere vya kuzuia uharifu wa watu wanaofanya makosa
mitandaoni lakini umekuwa na vipengere ambavyo anasema ndio vitakuwa vimeua Uhuru wa Habari nchini
Bi Liundi ametolea mfano kipengere cha
sheria kilichokuwepo kwenye mswaada huo ambacho kinamtia hatiani mtu anayetuma
picha ya matusi na vilevile kinamtia hatiani mtu anayepokea picha hiyo kwa
kusema kipingere hicho kinautata na kitawafanya watanzania wengi kuingia
hatiani.
Pamoja na hayo amebainisha kuwa kwa
sasa TGP wameshatoa matamko ya kumtaka Rais Kikwete asiweke sahini kwenye
mswaada huo.
Kwa upande wao Wamiliki pamoja na
waandeshaji mbali mbali ya Mitandao ya Kijamii nao wameendelea kumuomba Rais
Kikwete pia asiweke saini kwenye Maswaada huo wa Mwaka 2015 miongoni mwao ni
Evanc Bukuku ambaye ni Mmiliki wa Mtandao wa “Fullshangwe.Blogs”amesema
anaamini Rais Kikwete ni Mtu sikivu jambo ambalo anadai atasikia kilio cha
watanzania pamoja na wadau mbali mbali kutoweka saini kwenye mswaada huo.
Mbali na Bukuku mwengine ni Selemain Magari ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Fullhabari.blogs naye pia amemtaka Rais kikwete kutia saini mswaada kwa kusema utaliweka Taifa njia panda
Mbali na Bukuku mwengine ni Selemain Magari ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Fullhabari.blogs naye pia amemtaka Rais kikwete kutia saini mswaada kwa kusema utaliweka Taifa njia panda
No comments
Post a Comment