HABARI KUBWA LEO,SIRI YA CCM IMEFICHUKA,NI YA KUMFUKUZA MZEE MOYO SOMA HAPA KUJUA
SIRI ya
kufukuzwa mwanasiasa mkongwe nchini
na muasissi wa siasa za maridhiano Zanzibar, Hassan Nassor Moyo (pichani)ndani ya
chama cha mapinduzi CCM zimeanza kufichuka na sababu hiyo inadaiwa kutokana na uswahiba wake
wa karibu na Edward Lowassa.Mtandao huu umedokezwa),Anaandika KAROLI
VINSENT,Endelea nayo
Taarifa toka visiwani Zanzibar zinasema
Mwanasiasa huyo mkongwe kabisa ndani ya CCM ambaye alishiriki kukianzisha 5
Februari 1977,inadaiwa ukaribu wake wa Mbunge wa Monduli CCM,Edward lowassa
unadaiwa kumponza na sio madai ya usaliti wa kwenye chama hicho kama
yanavyosema .
Mzee Moyo alitimuliwa uanachama ndani ya
Chama hicho juzi kwa madai ya kung’an’ngania mfumo wa muungano wa Serikali tatu
ambao chama chake wamekuwa wakiupinga sana.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa
Mjini Magharibi, Aziza Mapuri alisema sababu ya kumfukuza mwanasiasa
mkongwe inatokana na kuzingatia Ibara ya 93(14) ya Katiba ya CCM.
Taarifa ambazo Mtandao huu ambazo umezipata
leo asubuhi na mapema zinasema sababu ya kufukuzwa Mzee moyo ambazo zinadaiwa
na CCM ni za uongo kwani sababu halisi ni inatokana na kuwa na ukaribu na
Mwanasiasa ambaye amekuwa akisumbua chama chake kutokana na nguvu aliyekuwa
nayo katika kutaka kuchukua nafasi ya Urais hapo baadae mwaka huu ambaye ni
Edward Lowassa.
Lowassa ambaye ni Waziri mkuu
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound ni miongoni mwa makada ndani ya CCM ambao
wanataka Urais kwa udi na Uvumba.
Akifichua sababu ya kumfukuzwa mzee Moyo
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) ambaye pia ni Mjumbe wa kamati CC kutoka visiwani Zanzibar,akiongea na Mtandao
huu kwa sharti la kutotaja jina lake amesema Chama chake kinaficha ukweli tu kwani
inajulikana wazi kwamba ukaribu wake na Lowassa ndio umemponza.
“Sikufichi bwana anachokizungumza bwana
Mapuri ni kuwadanganya watu tu ,kwani huyu mzee ni siku nyingi sana amekuwa
akishikilia msimamo wa Serikali tatu,iweje wamfukuze leo na sio nyuma,na sisi
tunajua kwamba huyo mzee aliaapa kumpigania Lowassa kuchukua nchi hii,ndio
maana wamemuengua mapema na hapa wanafanya ubabe tu”kimesema Chanzo hicho.
Mjumbe huyo amendelea kuongea kwa
uchungu anasema kwa sasa chama hicho chini ya Mwenyekiti Jakaya Kikwete ni kama
kinaongozwa kwa mfumo ambao anadai ni wa kibabe.
“Chama hichi kilipofikia sasa ni wazi
kinakuwa ni cha kibabe sana haiwezekani mtu ukimpenda mtu na ukimtaka agombee
Urais unapingwa na kufukuzwa uanachama,wakati wakiwa kwenye majukwaa wanasema
tuwashawishi tuwafuate watu wenye sifa na tuwaombe wagombee uongozi lakini
tukifanya hivyo tunabwanwa”ameendelea kusema.
Mzee
Moyo ambaye asili ya baba yake ni Songea, mkoani Ruvuma, mwenyewe akiwa
amezaliwa mjini Zanzibar, miaka 81 iliyopita, amekuwa na wake wawili, mmoja
mjini Zanzibar na wa pili jijini Tanga na ukaribu wake na Lowassa
unadaiwa kuchagizwa sana na kile kinachonekana mwanasiasa huyo kwamba lowassa atakuwa mtu mwajibikaji na
kukubali muundo wa Serikali tatu ambao Kada huyo mkongwe wa CCM anasema
unateweza kuwatoa wa Zanzibar kwenye mfumo kandamizi wa Serikali mbili.
No comments
Post a Comment