SEMINA YA TGNP: WAHARIRI WATAKA NGOS KUACHA KUWACHANGANYA WANANCHI, PINDA NAYE ASHAURIWA
Asasi za kiraia zimeombwa kuacha kuchanganya wananchi kuhusu katiba inayopendekezwa na badala yake wajikite katika kufafanua ukweli uliomo katika katiba hiyo ili kutoa uhuru wa kuamua maamuzi sahihi linapokuja suala la kupiga kura ,
Hayo yamebainishwa na wanablogger Tanzania wakati waliposhiriki katika semina maalum ya kuwajengea uelewa, kuhusu kura ya maoni ambayo hivi sasa inaonekana kuota mbawa kutokana na tume ya uchaguzi kutotaja tarehe rasmi ya kupiga kura hiyo,
Mmoja wa washiri hao, Bw Nathani Mpanagala ameonyesha mashaka yake juu ya kuchanganywa kwa wananchi na asasi mbalimbali, huku kila moja ikivutia kwake lakini ikishindwa kuonyesha ubaya wa katiba inayopendekezwa,
Mpangala amesema asasi kubwa lazima zifikie m,aafikiano nini wanataka kukileta kwa awalaji (Wananchi)vinginevyo hakuna kinachofanyika na rasilimali zitatumika bila ya faida,tuache kuwachanganya watu na tuwe wakweli aliongeza .
Suala la kuchanganywa kwa wananchi lilikuja kufuatia baadhi ya taasisi za kiraia kuwa na mtazamo wa kiukawa mara tu baada ya katiba inayopendekezwa kuwekwa mezani, watu wamegawanyika na hakuna ummoja tena wa kufikisha kero za wananchi na kuzisimamia,
Akitoa mafunzo kwa wanablogger, mwezeshaji toka mtandao wa jinsia TGNP Bw. Temba amesema wao kama TGNP hawaoni haya kusema aukweli juu ya katiba inayopendekezwa, na kuongeza kwamba ndani ya katiba hiyo mahitaji yao mengi yameingizwa.
Tumepiga hatua kubwa, mengi yameingizwa tena mazurio na kama utaniuliza mimi kati ya katiba inayopendekezwa na ile ya 1977 nitakwambia ni bora hii ya sasa, kwani imechukua mambo mazuri mengi.
Katika hatua nyingine, Mtandao wa kijinsia Tanzania kupitia wawezeshajai wake, wameishauri serikali kuacha kufikiri juu ya kuendesha michakato miwili ya kura ya maoni na kura ya viongozi kwani kutaleta shida kubwa kuanzia kampeni yake hadi kupiga kura yenyewe,
Tunajua kwamba kunampango wa serikali kuendesha kura ya maoni na kura ya viongzo siku moja, kama wanapanga hivyo ni bora wakaacha, italeta shida kwa wananchi na migogoro mikubwa,
Waziri mkuu Mizengo peter Pinda aliwahi kunukuliwa akisema wanaangalia uwezekano wa kufanya yote kwa pamoja, kwa hiyo muda uliopo watu watoe tu elimu kwa apiga kura.
No comments
Post a Comment