Zinazobamba

Nini Tufanye ili Allah atufanyie wepesi siku ya qiyama

 Na Selemani Magali
 Kuna mambo mengi sana ambayo sisi kama waislamu tunatakiwa tuyafanye ii tuweze kufikia lengo la kuumbwa kwetu na kuletwa kwetu hapa duniani, Miongoni mwa mabo hayo ni kama mfumo wa utoaji wa elimu ya dini, Mfumo wa upatikanaji wa vipaato vya halali kwa waislamu, mfumo wetu wa uchumi nk lakini mimi kwa upande wangu nimeona kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia mfumo wa utoaji wa elimu ya msingi ya dini ya kiislamu yaani MADRASA
Madrasa ni sehemu muhimu sana ambayo ndio inajenga misingi ya kupata jamii ya kiislamu yenye watu wanajitambua na kutambua umuhimu wao katika uislam, Madrasa zetu zimekuwa zikikabiliwa na matatizo lukuki ambayo pengine kutokanana kutotiliwa mkazo basi yemekuwa hayatatuliwi na kusababisha mizizi ya jamii isiyo na maadili kuendelea kurefuk
  • Chimbuko la tatizo.
a.Wasimamizi wa madrasa
Wasimamizi wa madrasa zetu wengi wao wamekuwa na matatizo yafuatayo
  • Baadhi yao si waaminifu hivyo imepelekea jamii ya wachangiaji kuhisi kucchangia ni sawa na kupoteza pesa bure
  • Wengi wao si wasomi na hawana upeo mkubwa wa masuala ya uongozi na usimamizi wa madrasa kulingana na wakati tulionao
  • Wengi wao hawana miradi ya kuwaingizia kipato hivyo kutegemea Madrasa ambazo nazo hazijitoshelezi,
  • Pia wengi wameingia woga wa kuwafuata watu wenye nacho ili wachangie maendeleo na program mbalimbali za madrasa.
  • Pia kutokana na sababu zilizotanguliwa Wasimamizi wmekuwa wakishindwa kuandaa program za kimaendeelo.
a.Wachangiaji wa maendeleo ya madrasa
Wachangiaji wa madrasa ambao ni wenye uwezo wa kuchangiwa nao wamekuwa na mtizamo hasi katika mantiki ifuatayo
  • Wamekuwa wakihofu kupoteza michango kwa kuwa na dhana kuwa wasimamizi wa madrasa si waaminifu
  • Hawajui tatizo la Madrasa ni kubwa kiasi gani
  • Hawajui wachangie nii?
  • Usiri juu ya Michango inayotolewa (kukosekana ka taarifa sahii juu ya matumizi ya fedha na michango)
  • Hawana Elimu ya kuchangia.
  • Hakuna Kinachowaunganisha Na Madrasa husika.

  • Tatizo la Jumla La Madrasa
  • Tatizzo kubwa la jumla lipo katika maeneo yafuatayo
    • Ukosefu wa vifaa muhimu katika madrasa kwa mfano misahafu, vikalio,majuzuu,Majengo chakavu, vitabu nk.
    • Kukosekana kwa posho na mishahara kwa watumishi wa Madrasa zetu
    • Ukosefu wa vitu vyenye kuwavuta watoto kwa mfano, kifungua kinywa, Madaftari,na vifaa vya kusomea.
    • Utoaji wa misaada kwa watoto mayatima na ambao hawana uwezo wa kimaisha.
    • Uwepo wa vitendea kazi kwa watumishi wa madrasa kwa mfano usafir, ofisi za kudumu nk,

    • Suluhisho la tatizo

    Suluhisho la moja kwa moja la tatizo hili ni kutafuta njia ambayo mchangiaji atatua tatizo moja kwa moja kwa kupata taarifa sahii juu ya tatizo husika, moja ya njia hizo ni Hii website unayosoma leo ambayo ina taaifa muhimu juu ya Madrasa zetu, sehemu zilipo, matatizo yanayozikabili nani muhusika nk. tunaamini kuwa kwa kusoma kwako website hii utaanza kuchangia ili dini yetu ipige hatua kupitia nguvu na jasho lako.
    Kwa msaada wa  http://www.muislamwakweli.net/index5.php

    No comments