HABARI KUBWA-ZITTO KABWE AENEZA UWONGO WAKE TENA,ATUMIA ZIARA YAKE KUUCHAFUA UKAWA MIKOANI,SOMA HAPA KUJUA
KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo,
Zitto Kabwe ameendelea kuwadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake katika Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumetokana na umakini wake wa kufuatilia
“mambo yanayowakandamiza wanyonge.” Anaandika Ditha
Nyoni, Songea …
(endelea).
Akihutubia mkutano wa hadhara mkoani
Ruvuma, Zitto amewadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake Chadema, kumetokana
na msimamo wake wa kutetea maslahi ya wananchi.
Amesema baada ya
kutambua baadhi ya viongozi wa Chadema hawataki kuwatumia wanyonge kwa kuwapigia
kura na kujipatia ruzuku, yeye wenzake wengine wameamua kuanzisha chama
kitakacho watetea wanyonge wakiwemo wakulima ambao nguvu zao zikiisha wanakufa
maskini.
Amedai kuwa yeye ndiye aliyeibua
hoja ya mkataba wa madini wa Buzwagi ambako waziri wa nishati na madini,
alifutwa kazi; hoja ya kumng’oa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa,
Operesheni Tokomeza, wanaoficha fedha nje ya nchi na sakata la Escrow.
Amewataka wananchi madai kuwa
yeye ni msaliti na kwamba wawapime wabunge wao kwa kazi walizozifanya.
Hata hivyo, katika yote
aliyoeleza Zitto hakuna hata moja ambalo ni kweli.
Mathalani, hoja
ya mkataba wa Buzwagwi, iliibuliwa na gazeti la kila wiki la MwanaHALISI;
katkka sakata la Buzwagwi, kinyume na madai yake, hakuna waziri hata mmoja
aliyefutwa kazi.
Aliyekuwa waziri wa nishati na
madini, Nazir Karamagi ambaye alisaini mkataba huo nchini Uingereza, alifutwa
kazi 18 Februari 2008, kutokana na kashifa ya maarufu ya Richmond.
Sakata la Richmond liliibuliwa
bungeni na Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya aliyekuwa mbunge wa
Bumbului (CCM), William Shelukindo.
Vilevile, kinachoitwa
“Operesheni Tokomeza,” kiliibuliwa bungeni na Christopher ole Sendeka, mbunge
wa Simanjiro (CCM).
Kamati Kuu (CC) ya Chadema, ilimfukuza
uanachama Zitto na wenzake watatu – Prof. Kitila Mkumbo aliyekuwa mjumbe wa CC
na Samson Mwigamba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha – kwa
madai ya usaliti, kusingizia viongozi wakuu wa chama na kushirikiana na maadui
wa chama.
Akisoma maamuzi ya
CC, tarehe 22 Novemba 2013, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto na genge
lake wametuhumiwa kwa makosa 11 ya usaliti, yaliyotokana na “Waraka wa Mabadiliko.”
Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Kitila, ulilenga kuteka
chama na kukikabidhi kwa maadui wa chama wakiwamo watu kutoka Idara ya Usalama
wa Taifa (TISS).
Zitto ndiye aliandaliwa kuwa
mwenyekiti wa chama hicho; naye akakiri kutaka kufanya mapinduzi ya uongozi
kinyume na katiba.
“…baada ya kumsikiliza Dk. Kitila, Kamati Kuu imebaini kuwa
mkakati huo haukulenga kumfanya Zitto kuwa mwenyekiti pekee, bali ulikuwa na
malengo makubwa ya kukibomoa chama hicho,” ameeleza Lissu.
Amesema, Zitto
alikihujumu chama hicho na kushiriki kujitoa kwa wagombea wake wa ubunge katika
majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini, Singida Mjini na kuwa mwaka 2006,
alipewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM).
1 comment
SIASA BWANA NYIE WOTE WASANII TU
Post a Comment