MASIKINI MREMA,KIGOGO WA CHAMA CHAKE AMKIMBIA NA KUHAMIA CHADEMA,SOMA HAPA KUJUA
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kyerwa mkoani
Kagera 2000-2005, Benedicto Mutungirehi, amekihama Chama chake cha Tanzania
Labour (TLP) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika
Mwandishi wetu … (endelea).
Mutungirehi ambaye ni mwanasiasa msomi,
amefikia uamuzi huo jana jimboni Kyerwa na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge
katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu.
Akiongozana na
wanachama wenzake 26 wa TLP, Mutungirehi alikabidhiwa kadi ya Chadema na mwenyekiti
wa chama hicho wilayani Kyerwa, Deus Rutakyamirwa.
Katika uchaguzi mkuu wa 2000, Mutungirehi alishinda kura za maoni
ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini akaenguliwa kwenye vikao vya uteuzi,
jambo lililowafanya wananchi wa Kyerwa kumlazimisha ahamie upinzani.
Baada ya kutii
sharti hilo, wananchi walimchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wao na hivyo
kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Justuce Katagira.
Hata hivyo, katika uchaguzi mkuu uliofuata mwaka 2005, Mutungirehi
aliangushwa na Katagira ambaye analishikilia jimbo hilo hadi sasa kutokana na
TLP kupoteza mvuto baada ya mwenyekiti wake, Augustine Mrema kuporomoka kisiasa.
Zimekuwepo juhudi za
muda mrefu sasa za wananchi wa Kyerwa kumshawishi Mutungirehi ahamie Chadema na
kugombea ubunge kutokana na chama hicho kujijengea mtandao mkubwa ambao unampa
uhakika wa kushinda.
Mutungirehi alirejea rasmi katika siasa za jimbo la Kyerwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo alikuwa mgeni rasmi kakika mkutano Ukawa uliofanyika Nkwenda stand na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Mutungirehi alirejea rasmi katika siasa za jimbo la Kyerwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo alikuwa mgeni rasmi kakika mkutano Ukawa uliofanyika Nkwenda stand na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Chanzo ni Mwanahalisi .online
No comments
Post a Comment