Zinazobamba

KUBWA-TANESCO KUZIMA MITAMBO YAKE,NI ILE YA AGREKO,IPTL,KILIO CHA ZITTO KABWE CHATIMIA,SOMA HAPO KUJUA


17
sehemu ya Mitambo ya Kinyerezi
 iliyotembelewa na wanahabari leo
SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO) liko mbioni kuizima mitambo yake ambayo inatumia mafuta mazito katika kuzalisha umeme, baada ya kukamilika kwa asilimia 84   mitambo yake mipya na ya kisisasa inayotumia Gesi iliyoko Tabata kinyerezi Jijini Dar es Salaam.Anaripoti KAROLI VINSENT,Endelea nayo
         Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja miradi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Simon Jilima wakati wa ziara na Waandishi wa Habari kwenye mitambo mbali mbali ya shirika hilo ambapo Mhandisi Jilima amesema mitambo ya kinyerezi imekamilika kwa asilimia 84 na inatarajia kukamilika kabisa hapo mwanzoni  mwa mwezi wa sita mwaka huu,ambapo-
         Anadai kukamilika kwa mitambo hiyo kutalisaidia shirika hilo kuachana na mitambo ambayo inatumia mafuta mazito ambapo anasema mitambo hiyo imekuwa mzigo kwa Tanesco kutokana na kupata hasara  kubwa za kununua mafuta za kuendesha mitambo hiyo.
       Mhandisi Jilima alibainisha kuwa kukamilika kwa mitambo ya kinyerezi  itapelekea kupatikana kwa  megawati 150 ambazo zitakwenda moja kwa moja kwenye Gridi ya Taifa.
    Vilevile amesema kukamilika kwa kabisa kwa mitambo inalifanya shirika hilo kuachana na makambuni ambayo yanaiuzia umeme shirika hilo ,yanaotumia mitambo ya mafuta.
        Aidha Mhandisi Jilima aliitaja mitambo hiyo inatumia mafuta mazito inayotarajiwa kuzimwa ni  ya Agreko na Symbion pamoja na  ya IPTL.
      Mtambo huo  wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu.
 Mbali na mitambo ya Kinyerezi,shirika la umeme nchini Tanesco pia linakamilisha vituo vyake mbalimbali vya kupoza na kusambaza umeme.vituo hivyo ambavyo waandishi mbali mbali wa Habari walivishuhudia, vipo katika hatua ya mwisho,ni kilichopo Gongo la Mboto jijini hapa,Kipawa pamoja na kilicho katika ya Jijini la Dar es Salaam karibu na mahakama ya Kisutu.
         Kwa mujibu wa Mkurugenzi  wa shirika la umeme nchini Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba anasema kukamilika kwa vituo hivyo ambapo vinatarajiwa kukamilika vyote mwishoni mwa mwaka huu anasema itasaidi kumaliza tatizo la umeme kwa sasa ambalo limetokana na mitambo ya sasa kwenye shirika la Tanesco kuchoka na kuelemewa uwezo.
     “Nataka niwaaambia wananchi wa Dar es Salaam kwa sasa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu,mitambo yote itakuwa imekamilika kwa asilimia 100,na kukamilika kwake kutasaidi kabisa kumaliza tatizo la kukatika umeme ambalo limekuwa kero kwa wananchi”amesema Mhandisi Mramba.
       Mhandisi Mramba ameongeza kuwa sababu ya kukatika umeme mara kwa mara ilitokana na mitambo ya shirika hilo kuchoka na kuwafanya wafanyakazi kuhangaika ila kwa mitambo mipya inayotarajiwa kukamilika anadai itakuwa ni ya kisasa ambayo inatumia teknolojia ya kisasa ya kumpyuta ambayo haitaitaji wafanyakazi wengi.

        Aidha,Mhandisi Mramba anasema mitambo  hiyo ya kisasa ni mizuri,mhandisi huyo amesema endapo kutatokea tatizo la kukatika kwa umeme sehemu kumpyuta ndio zitaonyesha na itapelekea kuondoa utaratibu wa sasa ambao unawafanya wananchi  kuripoti kwenye shirika hilo endapo umeme ukikatika.
   Kuzimwa mitambo ya umeme inayotumia mafuta mazito,itakuwa imemaliza kiu ya aliyewai kuwa mbunge wa kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambapo alipokuwa mbunge alikuwa anaitaka serikali kuachana na mitambo hiyo kutoka na kutumia pesa nyingi.

No comments