HABARI KUBWA-YAMEFICHUKA YA SAMWEL SITTA,NAYE ANAFADHILI CHAMA CHA KIPYA CHA CKUT,NAYE KAMA ZITTO KABWE,SOMA HAPA KUJUA

SIKU moja
kupita baada Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kukipa usajili wa mda
chama kipya cha Siasa cha kijamaa na uzalendo
Tanzania (CKUT)
‘’
siri zimeanza kufichuka kwamba chama hicho kinamilikiwa “kinyemela” na kigogo
wa juu wa chama cha Mapinduzi CCM’’.anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu
umezipata zinadai chama hicho
kinafadhiliwa kwa ukaribu sana na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta (pichani),kwa lengo
kwamba endapo mambo yakienda hovyo ndani ya chama chake cha mapinduzi CCM
kwenye wakati wa uteuzi wa mgombea wa Urais basi ajiwekee mazingira ya kukimbilia
huko.
“Hapa sio Sitta tu wako wengi wameanza
kujiweka mguu sawa kutafuta upenyo nje,na hapa watu wanasubilia tu maamuzi ya
Kamati kuu ya CCM wakati wakupitisha majina tu upande wa urais na NEC iamue na
hapa kuna kilauwezekano akapita mtu ambaye akipita tu chama kitakuwa na
msuguano ndani kwa ndani “
“Na watanzania waviangalie vyama hivi
vinavyoanzishwa kipindi cha Uchaguzi vingi vinakuwa ni vyama vya kimamluki tu
vya watu wapenda madaraka tu,”amesema Kiongozi wa CCM kutoka mikoa ya Kaskazini
Taarifa hizo zinakuja ikiwa teyari Mwenyekiti
na Muasisi wa Chama hicho cha Kijamaa na Uzalendo
Tanzania (CKUT),Ramadhani Semtawa kutangaza mara baada ya kupata usajili mda wakati wa mkutano na waandishi wa habari akisema wanamuomba Waziri Sitta kujiunga nacho kwani chama hicho wanadai kinaendana na Falsafa ya Ujamaa na kujitegemea iliyoasisiwa na Mwalimu Julias Nyerere.
Tanzania (CKUT),Ramadhani Semtawa kutangaza mara baada ya kupata usajili mda wakati wa mkutano na waandishi wa habari akisema wanamuomba Waziri Sitta kujiunga nacho kwani chama hicho wanadai kinaendana na Falsafa ya Ujamaa na kujitegemea iliyoasisiwa na Mwalimu Julias Nyerere.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wa Karibu wa Samwel
Sitta aliyezungumza na Mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina anasema Waziri huyo
anajihami ndani ya chama chake kutokana nguvu kubwa aliyonayo Kada mwenzake wa
CCM,Edward lowassa ambaye anaonekana kupewa nafasi kubwa ya Urais hapo baadae kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu
Kwa mujibu mtoa taarifa huyo anasema
kitendo cha lowassa kuchukua nafasi ya Urais kutamweka sehemu mbaya Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambapo amekuwa na mahusiano mabaya na Waziri
Mkuu huyo wa zamani.
Duru zinasema Chama hicho cha (CKUT),
kinachofuata itikadi iliyoijenga heshima Tanzania Miaka ya nyuma ya Ujamaa na
Kujitegemea zinasema uwenda chama hicho kikiushangaza ulimwengu baada ya
kutajwa kuwachukua Vigogo wengi wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanaojiona watakuwa na wakati mbaya akichukua
nafasi lowassa.
“Da mwaka huu mtashuhudia mengi sana,na
watu wameshaona nguvu ya Pesa aliyokuwa nayo Lowasa ni kubwa sana,sio pesa
teyari huyu bwana ameyateka makundi makubwa ndani ya nchi,yaani chama chake
kishapata presha,na hii itakuwa sawa na Rais Kikwete ilivyokuwa mwaka 2005 naye
alikuwa na magenge kama ya lowassa na alipingwa hivyo na kina mashishanga “,
“Na atapita tu huyu mtu,ndio maana wakina
Sitta wanahaha sana na mwaka huu sijui ccm kama itabaki salama”imeelezwa.
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli
na pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu kwenye Kashfa ya Ufisadi wa Kampuni tata ya
Richmound ambapo ni miongoni mwa makada wa CCM,wanaoutaka Urais kwa udi na
Uvumba.
Ambapo inadaiwa anauhasama mkubwa na samwel
Sitta unatokana na maamuzi ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge Dk Heririson
Mwakyembe yaliyomkaang’a mpaka akachukua uamzuzi kwa kujiuzulu ambapo mara kwa
mara lowassa amekaliliwa na Vyombo vya Habari akisema ameonewa na Kamati hiyo
kutoka na kutopatana na makada wenzake wa CCM.
1 comment
blog yenu inaongoza kwa uongo na habari za kutunga tunga tena zinatungwa nawatu ambao wanaupeo mdogo wa kufikiri
Post a Comment