Zinazobamba

HALI YA CHAKULA NCHINI NI SHWALI,WAZIRI WASIRA ASEMA SERIKALI IMEJIPANGA KUPAMBANA NA NJAA,SOMA HAPA KUJUA

pichani ni Waziri wa Kilimo,Ushirika na Chakula
Steven Wasia akifafanua jambo na waandishi wa Habari
picha na Maktaba

SERIKALI nchini imesema hali ya chakula katika maeneo mengi ya nchi kati ya mwaka 2014 na 2015 imeendelea kuwa imara kufuatia mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo katika kipindi hicho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
        Hayo yametengazwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika Steven Wasira wakati wa Mkutano na vyombo mbali mbali vya Habari ambapo amesema kulingana na Tathmini ya uzalishaji uliofanyika mwezi Agosti 2014 uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa mwaka 2013 na 2014 ulifikia tani 16,015,238 zikiwemo tani 9,828440 za nafaka.
         Waziri Wasira ameongeza kuwa mazao yasiyo na nafaka  yalikuwa tani 6,186,698,kwa mujibu waziri anasema uzalishaji huo ukulinganisha na mahitaji ya chakula ya tani 12,767,979 kwa mwaka 2014/2015.nchi ilikuwa na zaidi ya tani 3,247,359 za chakula ya ziada ya mahindi ambayo ilikuwa ni tani 1,547.570 na mchele ilikuwa tani 794,192.
         Amebainisha kuwa nchi ilijitosheleza kwa chakula kwa asilimia 125 ambapo,mikoa 23 kati ya 25 Tanzania bara ilibainika kuwa na kiwango vya ama ziada au utoshelevu na mikoa miwili tu ilidhihilika kuwa na uhaba wa chakula.
        Katika hatua nyingine Waziri Wasira amesema katika kipindi kinachoendelea cha Mwaka huu na mwaka 2016 kutarajiwa kuwa na uhaba wa chakula katika mikoa ya 10 ambayo imeoneka kutopata mvua kabisa ambazo anadai zimewakwamisha wakulima kufanya shughuli za kilimo.
      Waziri Wasira aliitaja mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Shinyanga,simiyu,Tabora,Mara,Kagera,Lindi Mtwara,morogoro,singina na katavi.
        Ambapo amesema jitihadi za Serikali ilizochukua katika mikoa hiyo ni kupeleka Chakula cha kutosha ili kuondoa Tatizo hilo.

               Vilevile Waziri Wasira amewataka wakulima kutunza akiba ya chakula  ili kujihami na balaa la njaa ambalo linaweza kutokea mbeleni.

No comments