Zinazobamba

PROFESA LIPUMBA ALIPUKA,AHOJI UWEZO WA KIKWETE KUSHINDWA KUPAMBANA NA MATATIZO,SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Profesa Lipumba akizungumza na wanahabari leo
Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa ni ukweli usipingika kuwa kwa sasa serikali ipo Taabani kutokana na mambo mengi yanayotokea huku serikali ikiwa haitoi majibu yanayowaridhisha
wananchi jambo ambalo limewafanya watanzania kukata Tamaa na nchi yao.Anaandika EXAUDI MTEI,Endelea nayo


         Akifungua kikao cha kawaida  cha baraza la uongozi Taifa la chama hicho mwenyekiti wa CUF mh IBRAHIM HAROUNA LIPUMBA amesema kuwa swala la sintofahamu juu ya mchakato wa uandikishwaji wa
daftari la kudumu la wapiga kura


     Pamoja na mchakato mzima wa upigaji kura imeonyesha wazi kuwa serikali ya tanzania imeshindwa kufanikisha zoezi hilo huku ikiitupia mzigo wote tume ya taifa ya uchaguzi ambayo na yenyewe imeshindwa 
         Amesema kuwa kushindwa kumalizika kwa uandikishwaji wa Daftari hilo kwa muda uliopangwa ni jambo ambalo lilikuwa haliepukiki kwani vyama vya upinzani pamoja na wadau mbalimbali
walishaitahadharisha serikali juu ya mchakato huo lakini serikali ilishindwa
           kusikiliza kilio chao na matokeo yake mchakato huo umeshindwa kuafanikiwa.

         Amesema kuwa moja ya ajenda za kikao hicho cha baraza kuu la uongozi la chama hicho ni pamoja na kujadili maswala hayo uyanayohusiana na kushindwa kufanikiwa kwa daftari hilo
la wapiga kura na kujadili nini cha kufanya ili uchagauzi uweze kufanyika na pia ufanyike kwa amani na upendo.


      Aidha Pr LIPUMBA amesema kuwa serikali ya tanzania imeshindwa kuwa sikivu kwa wananchi wake
ambao ndio waliowaweka madarakani huku akitolea mfano sakata la migomo ya wafanyabiashara,madereva na mambo mengine yanayoendelea ambapo amesema badala ya-
          serikali kukaa chini na watu hao ili kuwasikiliza imekuwa kinyume kwani wamekuwa wakitumia ubabe na kuwaacha walalamikaji hao kukosa la kufanya.

              Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ambaye ni Gwiji kwenye masuala ya Uchumi Afrika amesema kuwa kikao hicho cha kawaida cha baraza kuu la uongozi  la taifa ambacho kitaketi kwa siku mbili mfululizo  pamoja na mambo mengine watajadili muungano wa chama chao pamoja na vyama vingine vya upinzani umoja uliopewa jina la UKAWA
pamoja na kujadili ni jinsi gani ya kuimarisha umoja huo kuelekea uchaguzi ujao mwishini mwa mwaka huu.

No comments