HABARI KUBWA-CHENGE ALINUNUA JESHI LA POLISI,WAENDELEA KUMKUMBATIA SOMA HAPA KUJUA
JESHI la Polisi mkoani Simiyu,
limemkingia kifua Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge (pichani) (CCM), kwamba
bastola yake sio iliyotumika kufyatua risasi hewani kuwatisha wafuasi wa
Chadema kama inavyodaiwa. Anaandika Yusuf Katimba… (endelea).
Badala yake, Kamanda wa Polisi mkoa wa
Simiyu, Gemini Mushi, anasema “katika msafara ule kulikuwa na mtu anaitwa Ahmed
Ismail aliyekuwa na bastola. Alipiga risasi tatu juu ili kuwatawanya watu
wakaweza kuondoka.
Utetezi wa kamanda unakizana na ule wa wafuasi wa Chadema, wanaodai kuwa
Chenge-aliye pia Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali, aliwafuata katika ofisi
zao mjini Bariadi na muda mfupi baada ya kushuka kwenye gari, alifyatua risasi
hewani.
Madai
ya Chadema yametolewa na Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Vijana Taifa
(Bavicha), John Heche ambaye awali ndiye alihutubia wafuasi hao akiwa na Katibu
wa baraza hilo taifa, Julius Mwita.
Chenge
hakupokea simu yake kujibu madai hayo, lakini Heche amekiambia Chanzo changu
kuwa “baada ya kumaliza mkutano, wafuasi wa Chadema walitusindikiza kuelekea
katika ofisi za chama kusaini kitabu cha wageni.”
Heche ameongeza kuwa, wakiwa ofisini, Chenge
alifika eneo hilo na msafara wa wafuasi wa CCM wakiwa ndani ya magari kama sita
ambayo yalikuwa yakipiga nyimbo za kuisifu CCM, jambo lililowakera wafuasi wa
Chadema waliokuwa nje.
“Tulipoona
sintofahamu imeanza kutokea kwa wafuasi wa pande zote mbili, nikatoka nje na
kumwona Change anashuka katika moja ya gari. Niliamua kumfuata ili kumtaka
aondoke eneo hilo kwa walikuwa wamevamia msafara wetu bila sababu ya
msingi,”anasema.
Heche
anaongeza kuwa, “wakati namfuata Chenge kabla hata sijamfikia, alitoa bastola
na kufyatua risasi tatu juu, na hapo ndipo vurugu zilipoanza.”.
Anasema
kuwa hatua hiyo ilisababisha taharuki kubwa ya watu kukimbia hovyo, na hivyo
yeye pamoja na viongozi wenzake kulazimika kutoa taarifa kituo cha polisi na
kupewa Kumb namba BAR/RB/1195/2015.
Anafafanua
kuwa “jambo la ajabu, tulipofika kituoni, Chenge tayari naye alikuwa amefika,
lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.
Maelezo
ya pande zote yanaibua maswali kadhaa. Kwa mfano; ni wafuasi wa chama kipi
waliwafuata wenzao. Kwanini walifanya hivyo. Polisi waliotoa vibali vya
mikutano walikuwa wapi. Mfyatua risasi alitumia taratibu gani. Heche anamfahamu
Chenge au. Tumwamini Heche aliyeshuhudia tukio au kamanda aliyepewa taarifa?
Chanzo changu, hakikupata majibu ya kutosheleza kutoka kwa Kamanda
Mushi. Badala yake amesema, “kulikuwa na mikutano miwili; wa Chadema
uliofanyika kwenye uwanja wa Basketball na ule wa CCM uliofanyika Isanga
Kilometa 10 kutoka mjini.
Anasema
kuwa baada ya mikutano wafuasi wa vyama hivyo walitawanyika, na kwamba CCM
walipokuwa wakirudi mjini kupitia barabara kuu huku gari la Chenge lilikuwa
likipiga mziki tangu walipoondoka mkutanoni.
“ Walipofika
eneo linaloitwa Mwisho wa Lami karibu na ofisi za Chadema, Chenge alishuka
kuwasalimia watu ambao walikuwa wakicheza mziki akidhani ni wafuasi wa CCM, na
aliposhuka ndipo aliposikia amri ya ‘piga mawe’ na hivyo akarudi kwenye gari
lake,” amesema Mushi.
Alipoulizwa
uzito wa tukio na matumizi ya silaha za moto kama vinaendana, “amesema haoni
tatizo kwa kuwa risasi hazikumlenga mtu.Risasi ya moto inakuwa na matumizi
mabaya pale inapomlenga mtu. Sijaona hoja ya msingi hapo. Silaha ndogo ni ya
mtu kujilinda mahali popote.”
Amesema kuwa, silaha hiyo inamilikiwa na Ismail kihalali na kwamba
wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment