CHAMA CHA MREMA CHAZIDI VURUGIKA,USALITI WAKE WAKIMALIZA CHAMA CHAKE,CHAGEUKA CHA HARUSI,SOMA HAPA KUJUA
LICHA ya tambo za Mwenyekiti
wa Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Augustine Mrema kuwa ameombwa na Kamati
Kuu kutetea nafasi yake katika uchaguzi unaofanyika leo, baadhi ya wanachama
wanapinga mkutano mkuu wakidai wajumbe wake sio halali.Anaandika Pendo Omary… (endelea)
Mkutano huo, unafanyika katika Hoteli ya Kings Palace iliyopo Sinza
jijini Dar es Salaam ambapo kwa mujibu wa Mrema, wajumbe 120 kutoka mikoa yote
nchini walitarajiwa kuhudhuria.
Hata
hivyo, kauli ya Mrema inakinzana na baadhi ya wanachama wa TLP ambao wamekuwa
wakipingana naye kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kuwasilisha malalamiko
yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Akizungumza na Chanzo changu kwa niaba
ya wenzake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya TLP, James Haule
amesema “kinachofanyika leo sio mkutano mkuu labda kama ni genge la watu wako
kwenye harusi.”
Haule anafafanua kuwa “hatukushirikia mkutano huo kwa sababu hauna
wajumbe halali. Ili uweze kuwa mjumbe wa mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ya
TLP lazima uwe umechaguliwa na mkutano mkuu wa mkoa. Hili halikufanyika, sasa
wanachagua nini?”
Anasema kuwa hayo ndiyo malalamiko waliyofikisha kwa msajili wa vyama
kuhusu mgogoro ndani ya TLP na hivyo Mrema akaagizwa kuhakikisha uchaguzi mkuu
wa viongozi wa chama unafanyika kabla ya Aprili 24 mwaka huu.
Alipoulizwa
kama wamelalamika tena kwa msajili kuhusu uhalali wa wajumbe wa mkutano
unaoendelea. Haule amesema “Msajili anatuhadaa kwamba kama hatukubaliani na
uchaguzi tufungue kesi mahakamani, huku akijua kabisa kwa mujibu wa katiba ya
TLP, mwanachama akienda mahakamani anajifuta uanachama.”
“Sisi tunamtaka msajili wa vyama awajibike kwa hili, ajiuzulu kwa sababu
ndiye anambeba Mrema kukiuka katiba. Mimi naishi hapa Dar es Salaam, hao
wanaoitwa wajumbe wa mkutano mkuu ni ‘wahuni’ wa kuokoteza mitaani wamelipwa
posho na kupewa kofia na fulana,” amesema Haule.
Akijibu tuhuma hizo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa TLP, Mrema
amesema “kumezuka kikundi kinachojiita Kamati ya
Maridhiano ndani ya TLP, ambacho kinapinga uhalali wa marekebisho ya katiba ya
chama hicho ya mwaka 2009, uhalali wa uongozi uliopo madarakani na madai ya
kukiukwa kwa katiba.”
Mrema ambaye alitumia takribani asilimia 90 ya hotuba yake kulalamika kwa wajumbe kwa masuala yake binafsi ya ubunge wa Vunjo, amedai kwamba TLP ina migogoro ya aina mbili- moja ni ile inayohusu chama kwa ujumla wake na ule unaomhusu yeye pekee.
Mrema ambaye alitumia takribani asilimia 90 ya hotuba yake kulalamika kwa wajumbe kwa masuala yake binafsi ya ubunge wa Vunjo, amedai kwamba TLP ina migogoro ya aina mbili- moja ni ile inayohusu chama kwa ujumla wake na ule unaomhusu yeye pekee.
Amesema mgogoro unaomhusu yeye pekee
ni dhidi ya Abdulrahman Kinana – Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
James Mbatia – Mwenyekiti wa Chama cha NCCR – Mageuzi.
Mrema amesema 25 Machi 2015, Kinana alimkashfu na kumchafua na kumsingizia tuhuma za uongo kwamba anajilimbikizia madaraka yote, hakuna wa kumhoji na ni Mwenyekiti wa fedha za mfuko wa jimbo.
Mrema amesema 25 Machi 2015, Kinana alimkashfu na kumchafua na kumsingizia tuhuma za uongo kwamba anajilimbikizia madaraka yote, hakuna wa kumhoji na ni Mwenyekiti wa fedha za mfuko wa jimbo.
Ameongweza kuwa, kumekuwepo na
kampeni chafu ya kukifuta TLP kwenye jimbo la Vunjo na nchi nzima. Kampeni
alizodai kufanywa na NCCR – Mageuzi chini ya Mbatia; zilizopewa jina la “Delete
TLP/Mrema”.
“Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Makao makuu ya TLP, Getrudi Pwillah, aliasi na kujiunga na
“Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Makao makuu ya TLP, Getrudi Pwillah, aliasi na kujiunga na
NCCR – Mageuzi na yeye ndiye kuanzia
wakati huo amekuwa kinara wa kampeni ya Delete TLP,”amedai.
Kwa mujibu wa Mrema, mgogoro mwingine ni kuhusu Jeremiah Shelukindo – aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na kuasi kisha kuzira kuingia ofsini na kukataa kufanya kazi za chama.
Kwa mujibu wa Mrema, mgogoro mwingine ni kuhusu Jeremiah Shelukindo – aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na kuasi kisha kuzira kuingia ofsini na kukataa kufanya kazi za chama.
Amesema “kuna baadhi ya viongozi wa
mikoa wakiwemo madiwani hawafanyi kazi za chama na wamejiunga kwa siri/wazi na
njama za “Delete TLP”.Ushahidi uliopo, madiwani Yolanda Lyimo wa kata ya Kilema
Kati na Jesse Makundi wa Mwika Kaskazini, walinukuliwa na gazeti la Tanzania
Daima la Oktoba 2014 wakimpigia debe waziwazi jukwaani Mbatia.”
Mrema pia amezungumzia hali ya ulinzi na
usalama nchini kwa kusema kwamba hali ya siasa nchini sio nzuri, kutokana na
kuwepo matukio ya ugaidi, udini, mauaji ya albino, uvamizi wa vituo vya polisi
na migomo isiyokwisha.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalsi.oline
No comments
Post a Comment