Zinazobamba

CHUO KIKUU HURIA CHAZIDI KUKUA,SASA KUANZISHA "COLLEGE"YAKE,PFOFESA MBWETE AZIDI WEKA HISTORIA SOMA HAPA KUJUA

01
Pichani ni Profesa Mbwete

CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kipo katika mchakato wa kufanya maboresho ya mfumo wa utoaji wa elimu ambapo sasa kitaanzisha vyuo katika ngazi ya mkoa (College).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
         Katika mabadiliko hayo chuo hicho pia kitafungua matawi katika ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na   Halmashauri ya za wilaya.
              Makamu Mkuu wa OUT Profesa Tolly Mbwete ameeleza hayo leo alipokuwa akiongea na wana jumuiya ya chuo hicho katika mkoa wa Temeke ambao wamemuandalia sherehe ya kumuaga, kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyuo vikuu barani Afrika.
                  Amesema mchakato wa mabadiliko hayo tayari umepata Baraka za Tume ya Vyuo Vikuu nchini na kwamba muda si mrefu OUT itaanzisha college katika ngazi ya mikoa.
          Kwa upande wake Mkurugenzi wa OUT mkoa wa Temeke Dk. Jacquiline Bundala amesema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2007 chuo hicho kimepata mafanikio makubwa.
           Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka wanafunzi 258 waliokuwepo wakati huo hadi zaidi ya 600 waliopo sasa.
Pamoja na mafanikio hayo Dk. Bundala pia amesema chuo hicho mkoa wa Temeke kinakabiliwa na tatizo la mtandao ambao ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kujifunza.
           Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria mkoa wa Temeke Malimi Ntegwa ameutaka uongozi wa chuo hicho kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi ikiwemo tatizo la upatikanaji wa vitambulisho, sehemu za kujifunzia hasa wakati wa vipindi vya ana kwa ana.
mwisho


No comments