Zinazobamba

UKAWA YALIPULIWA HADHARANI, CHAMA ADC CHACHAMAA SOMA HAPA


Chama cha ADC kimechukua maamuzi magumu ambayo yameshindwa na vyama vya upinzani vingine kikiwamo chama cha mapinduzi, na umoja wa kutetea katiba  maarufu kwa jina la ukawa baada ya kuamua  wanachama wake kujikita dhaidi katika kusoma katiba inayopendekezwa ili siku ya kupiga kura waweze kuwa katika mazingira mazuri ya kuamua,

Akizungumza katika siku ya kuzindua Umoja wa wanawake wanaunda chama hicho, pamoja na umoja wa vijana wa chama hicho mapema hii leo, Mwenyekiti wa Chama hicho Tiaifa, Bw. Saidi Miraji, amesema Wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kuna haja ya wanachama wao kusoma katiba inayopendekezwa ndipo hapo wanatakuwa na uwezo wa kujua ni kitu gani kipo katika katiba na kama inawafaa wapigie kura ya ndiyo na kama wanaona itakuwa ni janga kwa taifa basi wapige kuya ya hapana,

Amesema Msingi wa kuruhusu watu wwasome katiba unajengeka katika maana ya kumpa mtu uhuru wa kuamua, huwezi wewe mtu mmoja unasoma katiba kisha unasema katiba haifa, huu ni ukiritimba na siasa ambazo si shirikishi ni vyema watu wakaachiwa kuamua wenyewe,
Aidha mkuu huyo wa chama ameendelea kusema kuwa, chama chake kitahakikisha kinasambaza katiba inayopendekezwa hadi vijijini kwa wanachama wake ili wapate fursa ya kuisoma na kutoa maamuzii,
Ndg Zangu nataka niwaambie kuw kukaa kimya na kususia mchakato si dawa, Kwa vyovyote vile katiba hii inayopendekeza itapigiwa kura, na maccm sasa ili tuweze kupambana nao lazima na sisi tusome katiba na tukaamue kwa kupitia kura, kura ndiyo silaha yetu aliongeza..
Hawa ambao wanaosema hawapigi kura wanaajenda yao na huwenda tayari wamepewa fedha ili wasije kur. Unawezaje kuja kukataa kupiga kura huku ukijua wazi kuwa usipopiga ni sawa na kubariki hiyo katiba, naamini watu watajitokeza kuja kupiga kura sasa wewe kama hutaki kwa nini usipige kura ya hapana,
Anasema watanzania wanadangaywa na huu umoja wa Ukawa na kusema khuenda wanalao wanalotaka kulitekeleza hivyo wakishiriki katika mchakato wa kura huenda mambo yasiwaendee vyema.

MWENYEKITI WA CHAMA cha ADC SAID MIRAJI ABDULLAH akifafanua kuhusu msimamo wa chama hicho katika sakata zima la katiba Pendekezwa, katika mkutano huo wa wanachama wa ADC mwenyekiti huyo amewataka wanachama wake kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini kisha waamue kwa kuipigia kura,Msimamo huo unakwenda kinyume na msimamo wa umoja wa kutetea katiba mpya Ukawa ambao tayari wameshaonyesha dhamira yao ya kususia mchakato mzima.
Wanachama wa chama cha ADC wakionyesha nakala za katiba pendekezwa mara baada ya kupewa na chama HICHO MAPEMA HII LEO, wANACHAMA WOTE NCHINI wa chama cha ADC wametakiwa kuisoma katiba Pendekezwa popote pale walipo ili waweze kuamua siku ya kupiga kura,Chama hicho kimewahakikishia wanachama wake kuwa kiko tayari kusambaza kopi za katiba hjiyo ili waweze kusoma na kuamua, amesema tayari wanakopi 10,000 ambazo wamepewa kuzisambaza kwa wanachama wao.
Sehemu ya Jumuiya ya wanawake ya chama cha ADC wakifuatilia mada am bazo zilikuwa zinatolewa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. Saidi Miraji Abdullah mapema hii leo
Naibu katibu mkuu wa chama cha ADC akifafanua jambo kuhusiana na Suala zima la kusoma katiba na msimamo wa chama hicho kabla mwenyekiti wa chama hicho Tiafa bado hajafungua mkutano wao, Katibu huyo ametumia fursa hiyo kuwataka jumuiya ya wanawake na jumuiya ya Vijana ya chama kuhakikisha kuwa wanajitokeza na kuchukua Fomu kwa wingi ili kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama, Ikiwamo nafasi ya Udiwani, Ubunge,na Urais

Katibu mkuu wa chama cha ADC akifafanua jambo mbele ya wanajumuiya ya wanawake ya ADC na ya vijana kuhusu mkakati wa chama dhidi ya uchaguzi ujao, na kuwataka kutoogopa kugombea nafasi mbalimbali katika chama.






No comments