Zinazobamba

TGNP WAJA NA KAMPENI YA KUENZI MICHANGO YA WANAWAKE WALIOFANIKIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Bi. Lilian Liundi moja ya kitabu ambacho kina majina ya wanawake waliofanikisha uhuru wa Tanganyika,akiwemo Bibi Titi, sasa mchakato umeanza wa kuibua wengine waliofanya makubwa katika nchi hii.

TGNP wametangaza kuwepo kwa KAMPENI ya kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika historia ya Tanzania itakayozinduliwa 27 Machi mwaka huu jijini Dareslaam,
Akizungumza na Mtandao huu Ofisini kwake,  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  Bi.Lilian Liundi amesema kuwa  Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuwaenzi wanawake wote waliofanya vizuri katika kuleta maendeleo kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa bila kujali ukubwa wa mtu.
Liundi ameendelea kusema kuwa, Dhamira ya kuwaenzi wanawake ambao wameonyesha mchango mkubwa kwa jamii inayowazunguka inatokana na ukweli kuwa mpaka hakuna utamaduni wa kutambua michango ya mashujaa wetu hususani wanawake
Katika kampeni hiyo itajikita katika kuwaenzi Wanawake wote wakiwemo  wale wanaojulikana na wasiojulikana lakini wamekuwa hawatajwi mahali popote katika historia ya nchi japo wana mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na kutengeneza historia ya nchi.  
Kampeni itasaidia kutafiti na kukusanya taarifa muhimu za michango ya wanawake katika maendeleo na historia ya nchi kijamii, kiuchumi na kisiasa, na hivyo kuwafanya wanawake watambulike kitaifa na kimataifa
Malengo mengine ni kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuibua na kutoa taarifa zilizopo na zitakazo kusanywa na kuzihifadhi katika makumbusho na sehemu nyinginezo kwa njia ya digitali na makala;
Kutumia taarifa hizo kuwaenzi wanawake kama sehemu ya kuhamasisha vizazi vya sasa na vijanvyo umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika maendeleo endelevu. Kuendeleza mijadala kuhusu michango na ushiriki wa wanawake na kudai uelekezaji wa rasilimali kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuendeleza ushiriki wanawake na kuwaenzi.
“Kampeni itakuwa na awamu tatu. Kilele cha awamu ya kwanza kitakuwa ni wakati wa tamasha la jinsia ambapo chapisho maalumu, makala ya video, onyesho maalumu vitaandaliwa. zawadi mbalimbali kwa wanawake watakaokidhi vigezo vinavyoonesha mchango mkubwa katika maendeleo na historia ya nchi zitatolewa,” ameongeza Liundi.
Kampeni hiyo itachukua miaka mitatu. Inatarajiwa kuhusisha wadau mbalimbali wakiwemo TGNP Mtandao, Makumbusho ya Taifa, Women Research Development Project, Women Fund Tanzania (WFT), Soma na Shule ya Uandishi wa Habari ya RAIDA pamoja na mashirika ambayo yanahusika katika kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia nayo pia yatahusishwa katika kampeni hii.

No comments