WAZIRI MKUU PINDA AUMBULIWA, JUKATA WASEMA KURA YA MAONI NI NDOTO KUFANYIKA
| Sehemu ya wanahabari wakisikiliza kwa makini, hoja za makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba, |
| Mdau akiwa kazini mapema hii leo. |
Kukiwa na kauli za sintofahamu ambazo zinatolewa naviongozi wa ngazi za juu akiwemo waziri mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Kayanza Petter Pinda kuhusu kura ya maoni, jukwaa la katiba limeibuka na mambo makubwa yaliyowashangaza wanahabari,
JUKWAA hilo la katiba wameibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda na sasa wamekuja na
tamko kali kwa selikali, wakiitaka kuacha mara moja nia yao ya kutaka kutumia daftari
la zamani kutumika katika upigaji wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi wanne
Tamko hilo limekuja kufuatia habari za kuaminika ambazo
Jukwaa la katiba imezinasa zikisema serikali inajiandaa kuendesha kura ya maoni
kama ilivyotangazwa na rais kwa kutumia daftari la kudumu la wapiga kura la
zamani, suala ambalo wanasema halikubaliki,
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema hii leo,
Kaimu mkurugenzi wa jukwaa hilo, Bw.
Hebroni Mwakagenda, amesema tayari wamepata taarifa hizo na kudai kuwa hatua
hiyo inafikiwa ikiwa ni nia ya serikali kutaka kulazimisha kura hiyo ya maoni
kufanyika katika tarehe iliyotangazwa,
Mwaka genda ameendelea kusema kuwa, kwa mujibu wa taarifa za
ndani toka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)iliyotolewa na mwenyekiti wake, Jaji mstaafu
Damian Lubuva zinasema daftari hilo la kudumu la mpiga kura kwa sasa
halitamaniki, kwani limechafuka vibaya mno kiasi cha kutoweza kurekebishika na
kutumika tena kwa kura ya maoni ya April 30,2015 kama ilivyotangazwa na rais.
Aidha, mwenyekiti huyo amebainisha uwezekano hafifu ambao
uliopo wa kufanyika kwa kura ya maoni, kwa kusema mpaka hivi sasa mchakato wa
kura hiyo uko katika mkwamo, kuanzia zoezi zima la uandikishaji, kutoa elimu,
na hata kupiga kampeni kwani mpaka hivi sasa siku zimebaki takribani 36 ambazo
hazitoshi kwa mchakato kukamilika,
Ameiomba serikali kuangalia upya sakata hilo, katika
mwelekeo wa kuahilisha , ili kutoa fursa kwa michakato mingine kufanmyika
ikiwemo uchaguzi mkuu wa oktoba ambao hivi sasa joto lake tayari limeshapanda
Akitaja sababu za kuahirisha
mchakato huo kwa wanahabari wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam
kaimu huyo mwenyekiti wa jukwaa amesemani kusuasa sua kwa zoezi la
uandikishwaji wa daftari la kudumu kwa mfumo mpya wa BVR,
Amesema hiyo ni ishara tosha kuwa ni ndoto kwa Tanzania kupata
katiba bora kwani hadi sasa kuna idadi kubwa ya wananchi ambao
hawajajiandikisha katika daftari hilo huku muda wa kupiga kura hiyo ukiwa
unakaribia jambo ambalo limekuwa likimtatiza kila mtanzania kama jambo hilo
linawezekana.
Amesema kuwa kutokana na upungufu wa vifaa pamoja na
rasilimali nyingine unaoonekana wazi katika zoezi hilo ni wazi kuwa daftari
hilo haliwezi kukamilika na kutumika katika kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa
Akizungumzia zoezi ambalo lilifanyika katika miji ya makambako na
njombe la uandikishwaji wa daftari la
mpiga kura limeonekana kuchukua zaidi ya miezi miwili kukamilika ambapo amehoji
ni vipi zoezi hilo linaweza kufanyika
kwa tanzania nzima ndani ya kipindi kifupi na kufanikisha kwa zoezi la upigaji kura ambao umepangwa
kufanyika tarehe 30 mwezi wanne mwaka huu.
Pinda alikaririwa na vyombo vya habari mbalimbali akisema kura ya maoni iko palepale, na watu wawe tayari kwenda kujiandikisha ili wapate fursa ya kuandika katiba inayopendekezwa.
No comments
Post a Comment