Zinazobamba

MSIMU WA PASAKA : HUWAWEI WAJA NA SIMU YA AINA YAKE, UKITABASAMU INAKUPIGA PICHA YENYEWE

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya huwawei Bw. Samson Majwla akizindua simu mpya iliyopewa jina la Y520 KISHKWAMBI mapema hii leo, Simu hiyo mpya ambayo inaingizwa rasmi sokoni ina kila kitu na kwamba bei yake ni sawa na bure. Anayemuangalia kwa karibu ni afisa bidhaa wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi huyo akifafanua zaidi juu ya ubora wa simu hiyo mpya iliyoingia sokoni, Majwala amesema simu hiyo inauwezo mkubwa ikiwemo uwezo wa kutunza betri kwa takribani masaa 24, kwa wale wanaotumia sana,kamera yenye ukwa wa MP5 nyuma na mbele ikiwa na MP3  inauwezo wa kupiga picha katika nyuzi 180" PARANOMA" NI MBOMBA NI YAKO

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni  ya Huwawei, akifafanua zaidi kuhusu kamera ya nyuma ya simu hiyo



Nafafanua, SIMU hii ni mbomba na zawadi katika msimu huu wa pasaka, wapenda chukueni fursa kwa kuitumia na mtakubali ubora wake.


Wanahabari wakiwa makini wakifuatilia uzinduzi huo wa Huwawei Kishikwambi, Mzigo ndo huo umeingia sokoni na kwa mara ya Kwanza watanzania watapata fursa ya kununua simu hiyo kwa njia ya M-pesa. Ukinunua kwa M-pesa utapata punguzo
Ni kama zawadi kwa watanzania, Kampuni ya kimataifa ya Huwawei katika msimu huu wa pasaka wamekuja kivingine na sasa wameibuka na simu mbona waliyoipa jina la Y520 KISHIKWAMBI ambayo inauwezo babu kubwa ikiwemo uwezo wa kipekee wa kupiga picha pindi unapoitabasamia,

Akizindua simu hizo mapema hii leo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa mauzo na masoko wa bidhaa hizo, Bw. Samson Majwala amesema Simu hiyo imetengenezwa ili kukidhi mahitaji ya wateja ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji huduma hiyo,

Majalwa ameendelea kusema kuwa simu hiyo ambayo inatumia laini mbili ni simu bora ambayo kioo chake kimetengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu huku kamera yake ikiwa ya kipekee ambapo inauwezo wa kupiga picha kwa kuitizama tu,

Simu hiyo ambayo Mtandao huu umeziona, inakaa na chaji kwa muda mrefu, huku ikiwa na uwezo wa kupiga picha za Nyuzi 180 tena kwa ubora wa hali ya juu,na kuongeza kuwa ni suluhisho kwa wateja vijana na hata wa rika zote nchini Tanzania

Akizungumzia upatikanaji wa Simu hizo , Majwala amesema simu hizo zitakuwepo katika maduka yote ya simu nchi nzima na cha ziada ni kwamba pia simu hizo zitapatikana katika maduka ya Vodacom ambayo zitauzwa kwa punguzo la bei kwa wale watakao nunu kwa njia ya Mpesa.

"Simu hizi zitasambazwa maduka yote ya simu nchi nzima, na kama unavyoziona zina kamera ya nyuma yenye MP5 na ile ya mbele ina MP3 ambayo ukiangalia tu ama kutabasamu basi inauwezo wa kupiga picha bila hata ya kuigusa" Aliongeza Majwala,

Simu hiyo ambayo imezinduliwa leo kwa wanahabari pia inatarajiwa kuzinduliwa tena kwa jamii huko COCO Beach ambako siku hiyo simu itauzwa kwa punguzo la bei ya hali ya juu na kwamba katika uzinduzi huo utahusisha wasaniimbalimbali wenye majina makubwa hapa nchini.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo wa masoko wa Huwawei ametoa wito kwa wananchi wa kitanzania kuamini bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo kwani kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha inatoa bidhaa iliyobora kwa watanzania na dunia nzima kwa ujumla yake.

No comments