Eti DIAMOND PLATINUMZ NYUMBA YAKE INAGHARAMA YA MILION MIA NNE" 400MIL"
Eti
inadaiwa kuwa mjengo wa mwanamziki mchanga ambaye amepata mafanikio ya haraka
kupitia mziki wa Bongo fleva hivi umemghalimu zaidi ya Tsh Milioni 400 mpaka
sasa
Mjengo huo wa Diamond uliopo maeneo ya Madale nje kidogo ya Jiji la Dar, unadaiwa kufikisha thamani hiyo kutokana na kuwa na vyumba vinne vya kulala, bwawa maalum la kuogelea (swimming pool), sehemu ya mazoezi (Gym), jakuzi, kaunta ya vinywaji, ukumbi wa kuchezea, studio ya muziki, uwanja wa mpira wa kikapu na sehemu ya kuchezea mchezo wa mishale (Darts).
Kwa mujibu wa Diamond, nakshi
za dhahabu alizoziweka katika kuta za bafu na chooni pekee, zimemgharimu sh.
mil. 70 kitu kinachoendana na utabiri wa mkandarasi huyo kuwa nyumba hiyo
inafikia thamani ya zaidi ya sh. mil. 400.
Akiuzungumzia
mjengo huo baada ya kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake
lichorwe gazetini, alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani
umechukua nafasi kubwa, na ‘material’ yaliyojengea ni ya gharama.
”Ukitazama kwa makini, material nyingi zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea,” alisema mkandarasi huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zinazonyesha.

source nimeitoa sehemu.

No comments
Post a Comment