HABARI KUBWA-CUF YAMUUMBUA ZITTO,YASEMA AMEJIUA KISIASA MWENYEWE SOMA HAPA KUJUA

CHAMA cha
Wananchi CUF ni kama kimemshukia Aliyewai pata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe (pichani) kwa kusema ni mwanasiasa jeuri ambaye hana maana ana anafaa kupuuzwa.Anaandika
KAROLI VINSENT.endelea nayo.
Zitto Kabwe ambaye amejiuzulu
Ubunge mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuepuka aibu ya kufukuzwa Ubunge na Spika wa Bunge Anna Makinda baada
ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kumfukuza uanachama wa chama hicho baada kutupiliwa mbali kesi yake mahakamani aliyoifungua-
Kupinga
maamuzi ya kamati kuu ya Chadema yaliyomfukuza kwenye chama hicho kutokana na
kudaiwa kwake kuandaa mipango ya kuwapindua viongozi wa wakuu wa chama hicho.
Kabwe ambapo
siku moja baada ya kujiuzulu amejiunga na chama cha ACT-Tanzania ambacho inadaiwa alikuwa nakimiliki 'kinyemela"tangu mwanzo
Akizungumza na Mwandishi wa mtandao
huu Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Abdual Kambaya mda huu kwenye
makao mkuu ya chama hicho yaliyopo Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo
mengine alizungumzia hali ya kisiasa ya Zitto Kabwe kwa kumtabilia mwanasiasa huyo kupotea kwenye
medani ya kisiasa nchini.
“Mimi namfahamu zitto kuwa ni mtu
makini sana tena mwenye maono makubwa,lakini kitendo chake alichokifanya cha
kuhamia ACT ni wazi amejiharibia kabisa kwani hata iko chama alichokwenda
hakina viongozi wenye uwezo wa kujenga chama,kwa mfano Katibu wa ACT mwigamba
ni mtu ambaye amezoea siasa za hovyo na sidhani kama atafika mbali na chama
hicho”amesema Kambaya.
Kambaya ameongea kuwa kitendo cha
zitto kabwe kuhama chadema kilionekana tangu mwanzo kwani amedai mwanasiasa
huyo ni kiburi na asiyeweza kushaurika.
“ Kama mtu makini sana ukimuangalia
zitto utamgundua ni mtu mwenye tabia ya kujiona na hiyo imetokana na yeye
kujikuta yuko juu baada ya kulewa sifa kutoka kwa wananchi na sababu hiyo ndio
inamuharibia sana na hawezi fika mbali “
“Na atafuata nyayo za wanasiasa kama
wakina Mrema yuko wapi leo na alikuwa anawafuasi wengi kuriko yeye hebu
jiulizeni leo vipi”ameongeza Kambaya.
Katika hatua nyingine Chama cha CUF
kimeitaka serikali kuacha tabia ya kung’ang’ania kura ya maoni ya kupitisha
katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la Katiba kufanyika tarehe 30 April mwaka huu, kwa
kusema hakuna uwezekano wa kufanyika-
kwa
tarehe kwa madai tume ya Uchaguzi nchini (NEC) imeshindwa katika zoezi lake la
kuwaandikisha wananchi kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya
wa (BVR)
Akizungumza kwa niaba ya chama cha CUF, Mkurugenzi huyo wa Mawasiliano wa Chama hicho Abdual Kambaya amesema kwa sasa ni wazi serikali inajidanganya kufosi kura ya maoni kufanyika tarehe hiyo .
Akizungumza kwa niaba ya chama cha CUF, Mkurugenzi huyo wa Mawasiliano wa Chama hicho Abdual Kambaya amesema kwa sasa ni wazi serikali inajidanganya kufosi kura ya maoni kufanyika tarehe hiyo .
No comments
Post a Comment