PROFESA LIPUMBA AWASUSA ACT-TANZANIA,AWATOLEA 'NJE'MKUTANO WAO.SOMA HAPA KUJUA
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof.
Ibrahim Lipumba, amekacha uzinduzi wa chama kipya cha ACT- Tanzania, anaripoti
Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa kutoka
kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, Prof. Lipumba amekacha
kuhudhuria uzinduzi wa ACT kwa kile kilichoitwa, “hofu ya kuchafuka.”
“Prof.
Lipumba hakuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya mahusiano yake na Chadema,
ambacho ni moja ya vyama vinavyounda UKAWA,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi
wa CUF.
Chama cha ACT,
kinaundwa kwa asilimia kubwa na waliokuwa viongozi na wanachama kutoka Chama
cha Demokrasia na Maendeleo.
Prof. Lipumba
alikuwa miongoni mwa wasomi wa ndani na nje ya nchi walioalikwa kutoa mada
katika uzinduzi wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaa, leo 29 Machi
2015.
Mbali na Prof.
Lipumba, wengine ambao wamekacha uzinduzi wa ACT-Tanzania, ni Samia
Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa
Ghana, Osagyefo Kwame Nkrumah.
Katika orodha
hiyo, walitajwa kuwamo pia, Ababu Namwamba-Katibu Mkuu wa Chama cha ODM cha
Kenya; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya;
mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini; kiongozi wa vyama rafiki vya
Ujerumani, Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto Progressive
Alliance.
Wachambuzi wa
mambo ya kisiasa wanasema, hatua ya Prof. Lipumba kutohudhuria uzinduzi wa
mkutano huo, unaashiria kutokubaliana na uadilifu wa waanzilishi wa ACT.
Aidha, hatua ya
Prof. Lipumba kususia uzinduzi wa ACT, yaweza kuwa imesukumwa na kutaka
kuimarisha umoja ndani ya UKAWA.
ACT kimezindua ilani
yake ya uchaguzi, kutangaza viongozi; na kudai kuwa kitarejesha Azimio la
Arusha, ambalo lilikufa kabla ya muasisi wake, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, akiwa bado yuko ulimwenguni.
Chanzo ni
mwanahalisi.onlie
No comments
Post a Comment