Zinazobamba

DC MAKONDA AMVAA ASKOFU GWAJIMA,ATANGAZA KIAMA NAYE SOMA HAPA KUJUA


NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kutangaza kuwakamata watu 15 ambao waliokuwa wakitaka kumtorosha Askofu wa Kanisa la Ufufo wa Uzima  Josephat Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam kutokana kuugua gafla akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisi
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (pichani) ameibuka na Kumtaka Askofu Gwajima kujisalimisha  ofisi kwake mara moja kabla hajamchukuli hatua kali za kisheria
        Kauli hiyo ya Makonda ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati wa akizungumza na mtandao huu ambapo amesema tayari ameshatoa maagizo kwa askari wake zaidi ya ishirini kumtafuta Askofu huyo popote alipo ilia achukuliwe hatua kali  kutokana na madai anayodai kwamba kiongozi huyo wa kiroho anamiliki silaha kinyume na taratibu.
       “Mimi teyari nimewaagiza askari wangu wamtafute popote alipo na wamfikishe ofisini kwangu ili mkondo wa sheria uchukue hatua kali,Maana sababu ya kumtaka ajisalimishe kwangu inatokana na kubaini –“
“Askofu huyu  anamiliki Bastora kinyume na taratibu tena hata mimi mkuu wa wilaya ambaye ndio mwenyekiti wa ulinzi wa wilaya hii sina taarifa,”amesema Makonda.
       Makonda ameongeza kuwa mbali na kumiliki Bastora hiyo pia amedai kwamba kiongozi huyo wa dini ametoa maneno ya kumkashifu Askofu wa Kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo ambapo amesema kauli hiyo inalengo la kuharibu na kuvunja amani ya nchi.
      Aidha,Makonda ameendelea kusema kwamba endapo askofu hiyo akikaidi kujisalimisha ofisini kwake basi ajiadhari kutafutwa kwa kunguvu na kuchukuliwa hatua kali.
     “Mimi ni mtu makini sana na hata chama changu wananijua na misimamo yangu kabisa na huwa sipendi kuyumbishwa namuomba Askofu Gwajima asilete utoto wa kupuuza maagizo yangu maana nitamchukulia hatua kali za kisheria”ameongeza Makonda

     Kauli ya Makonda inakuja ikiwa siku moja kupita baada maaskofu na waumini wa kanisa hilo kutoka mikoa mbalimbali, kuwasili jijini Dar es Salaam ili kufuatilia afya ya kiongozi wao.
        Waumini hao walianza kujitokeza jana saa 2 asubuhi katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ambako ndiyo makao makuu ya kanisa hilo.
        Hali katika uwanja huo, ilikuwa tulivu huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na watu wote ambao walionekana si             waumini wa kanisa hilo, wakiwamo waandishi wa habari wakibainika mapema.
          Ilipofika saa 5:30 asubuhi, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Gwandu Mwangasa alianza kuwatambulisha maaskofu na wawakilishi waliotoka mikoa mbalimbali ili waweze kutambuliwa na waumini wenzao.
          Mchungaji Mwangasa, aliitaja mikoa ambayo viongozi na maaskofu wamefika Dar es Salaam kuwa ni Lindi, Geita, Shinyanga, Mwanza, Morogoro na Iringa.
Mikoa mingine, ni Singida, Arusha, Tabora, Njombe, Tanga na Dodoma.
      Katika ibada hiyo, baadhi ya waandishi wa habari na wapiga picha walifukuzwa na viongozi wa kanisa hilo kwa madai kuwa hawana kibali cha kuwepo mahali hapo.

No comments