Zinazobamba

HABARI KUBWA-MKE WA DK SLAA AMUENYESHA KAMANDA KOVA,AHOJIWA KWA SAA TATU.SOMA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbDeFlzVS5srl3YR6UZ6K8WmgH8ViFRIqfrh5G-sU7gVc11NWSzuI-rBwDP0w35gE-lkhoYgnAHUYncjEYkuGyy232Zm8ECxR3AXAvV11TFeETxGQpVU2eGWJk0SyGzMhr9PJQQpRrJrp9/s1600/3.jpg

MKE wa Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa, mama Josephine Mshumbuzi amejisalimisha kwenye Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam na kushikiliwa kwa zaidi ya saa tatu kwa mahojiano.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
     Mama Mshumbuzi amejisalimisha leo makao makuu ya Jeshi la polisi kanda hiyo ili kutoa ushahidi juu ya tuhuma zilizoibuliwa na Chadema kuhusu mipango ya kumuua katibu huyo wa chadema ambazo wanadai kusukwa kwa ustadi mkubwa na Aliyekuwa Mlinzi wa Dokta Slaa, bwana Khalid Kagenzi pamoja-
       Na kaimu mkuu wa Usalama wa Taifa wa wilaya ya kinondoni Elisifa Ngowi pamoja na vigogo mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi CCM.
          Mwanamama Mshumbuzi aliwasili polisi majira ya saa nne asubuhi leo huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chadema,katika mahojiano hayo yaliyodumu zaidi ya saa tatu yanatajwa yalikuwa yanalengo kuchua ushahidi juu ya tuhuma hizo za mauaji.
           Kujisalimisha huko kwa Mke wa Dokta Slaa kunakuja ikiwa teyari jeshi hilo la polisi kanda ya Dar es Salaam limeutangazia ulimwengu kwamba idara ya Usalama  wa Taifa kutohusika kwenye madai ya mipango ya kumuua Dokta Slaa.

       Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova waliwambia wanahabari wiki iliyopita kwamba katika sakata hilo watahojiwa watu wote ambao wametajwa kuhusika kutaka kumuua Dokta Slaa ila kasoro usalama wa Taifa.

No comments