MAKONDA AANZA NA 'BONGO STAR SEARCH' YAKE KINONDONI SOMA HAPA KUJUA

MKUU wa
wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (pichani)amezindua shindano la “Kinondoni Talent Search”ambao
ni mpango wa wenye lengo la kutambua vijana wenye vipaji mbalimbali ili
kuwapatia nafasi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Makonda amezindua Shindano hilo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na vyombo mbalimbali vya habari ambapo
amesema shindano la Kinondoni Talent Search lina lengo la kuwatengenezea nafasi
ya mafanikio vijana wenye vipaji ,kuwapatia mafunzo muhimu ikiwemo
kuwaunganisha na wadau mbali mbali.
Makonda ameongeza kuwa Shindao hilo
ambalo litachukua mwezi mmoja na nusu
ambapo litashirikisha kata zaidi ya 30 zilizopo wilaya ya Kinondoni.
Aidha ,Makonda amesema katika hatua za
kuwatafuta vijana hao wenye vipaji, shindano hilo litasimamiwa na Jumanne Mrimmy
ambaye ni Afisa utamaduni wilaya ya kinondoni,Sebastian Mhowera afisa Habari wa
manispaa hiyo.
Mbali na viongozi wa Wilaya hiyo pia
manispaa hiyo imewahusisha wasanii mbali mbali ambao ni Peter Msechu,Jokate
Mwegelo pamoja na Mc anayetamba hapa mjini ambaye anatamba na mambo ya
uchekeshaji maarufu kwa jina Mc-Pilipili.
Vilevile Makonda amewataka Vijana
kujitokeza kwenye mashindano hayo yanayoanza hivi sasa na kujitokeza kwenye kata
zao zilipo wilaya,amesema mashindano hayo yanalengo la kuwatoka katika hali
ngumu ya maisha.
No comments
Post a Comment