HABARI KUBWA-UKAWA WATOKA MAFICHONI,WASEMA NENO ZITO,SASA NI KUTOA MGOMBEA WA KUTIKISA NCHI,SOMA HAPA KUJUA
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa umoja huo uliomalizika jana. Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi.Picha na Mwinyi Sadallah.
KWA
UFUPI
·
Tamko
hilo lilitolewa na viongozi wakuu wa Ukawa baada ya kumalizika kwa kikao cha
siku mbili kilichofanyika Shangani, Zanzibar kujadili hali ya kisiasa na
utaratibu wa kuwapata wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na
urais.
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema kila chama ndani ya
umoja huo kiko huru kutoa fomu na kuandaa wanachama wake watakaoshindanishwa
katika mchakato wa kuwapata wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Tamko hilo
lilitolewa na viongozi wakuu wa Ukawa baada ya kumalizika kwa kikao cha siku
mbili kilichofanyika Shangani, Zanzibar kujadili hali ya kisiasa na utaratibu
wa kuwapata wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na urais.
Mwenyekiti mwenza wa
Ukawa, Freeman Mbowe alisema wagombea wa umoja huo watapatikana kwa kuzingatia
sifa na uwezo wa kila mmoja na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko katika nchi.
“Hakuna chama
kinachozuiwa kutoa fomu kutafuta wagombea katika mchakato wa ndani wa chama
kabla ya Ukawa kufanya uteuzi wa mwisho,” alisema Mbowe ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chadema.
Kuhusu
mvutano
Kauli ya Mbowe
inakuja wakati kukiwa na wasiwasi miongoni mwa wanachama na wajumbe wa kamati
ya ufundi ya Ukawa kutokana na mvutano wa kila chama kutaka majimbo fulani
ambako kila kimoja kinadhani kinakubalika.
Hata hivyo, Mbowe
alisema Ukawa inaendelea kuimarika tangu kuasisiwa kwake na hakuna mpasuko kama
inavyodaiwa na baadhi ya watu.
“Hakuna mushkeli,
uhusiano wetu Ukawa unaendelea kuimarika na tutahakikisha tunasimamisha mgombea
mwenye sifa na uwezo wa kutuletea ushindi, hatutagubikwa na masilahi ya vyama,
tunataka masilahi ya Ukawa kwanza vyama baadaye.
“Ni ndoto Ukawa
kumeguka kwa sababu tumetambua umoja ni nguvu na wenzetu wanasubiri kuona
tunameguka,” alisema Mbowe katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Gharama
za uchaguzi
Alipoulizwa kuhusu
gharama za uchaguzi ndani ya Ukawa, Mbowe alisema ni mapema kueleza hilo lakini
hawatarajii kumwaga fedha kama wanavyofanya baadhi ya wagombea wa chama tawala
katika kutafuta nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais wa Muungano...
“Ukawa tunajiamini, tuna uwezo wa kushinda dola.”
Awali, Mwenyekiti
wa CUF ambaye pia mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema
kikao hicho kimepata mafanikio makubwa na kusisitiza kuwa wagombea wa Ukawa
watatangazwa baada ya kukamilika mchakato ndani wa vyama.
Alisema kwa
mwelekeo wa kisiasa baada ya kufanya tathmini, Ukawa ina nafasi kubwa ya
kuingia Ikulu ya Muungano na Zanzibar mwaka huu kutokana na CCM kushindwa
kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Alisema lengo
kubwa la Ukawa ni kuwa na Tanzania mpya yenye maendeleo na sera ya maisha bora
kwa Watanzania wote na kuwataka wananchi kuwa tayari kuyapokea mabadiliko ya
kiutawala baada ya Uchaguzi Mkuu.
Mwenyekiti wa NLD,
Dk Emmanuel Makaidi alisema chama chake si msindikizaji katika Ukawa na nia
yake ni kuona mabadiliko ya kiutawala yanatokea. Aliwataka Watanzania kuwa
tayari kufanya uamuzi mgumu.
“Tayari nimeota
ndoto Ukawa wanakamata madaraka ya nchi mwaka huu,” alisema Makaidi.
Katiba
mpya
Akizungumzia Kura
ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa, Mbowe alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), haiwezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja na kutaka Kura ya Maoni
isitishwe kwa sababu muda wa maandalizi ni mdogo na imeshindwa kuandikisha
wapiga kura kutokana na ukosefu wa vifaa.
Alisema Serikali
kuendelea kulazimisha Kura ya Maoni wakati matayarisho ni mabovu kutasababisha
vurugu.
Chanzo ni
Gazeti la mwananchi
No comments
Post a Comment