KAMPENI YA KUTAMBUA NGUVU ZA MWANAMKE KATIKA UKOMBOZI WA TAIFA LA TANZANIA YAZINDULIWA
Ile kampeni ya kutambua na kuenzi mchango na nguvu za
wanawake katika historia ya taifa la Tanzania imezinduliwa limezinduliwa mapema
hii eo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa sanaa za jukwaani, Makumbusho ya
Taifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bi.
Adelaide Sellema , amesema “katika historia ya taifa, ni mara ya kwanza kufanya
kazi maalum ya kutambua historia ya wanawake katika jamii kwa malengo ya kuweka
kumbukumbu sahihi kwa maendeleo ya historia ya Tanzania kwa vizazi na vizazi”.
Amesema, kwenye siasa na harakati za
ukombozi wa Tanzania, yanatajwa majina ya Mwani Theresa Ntare- aliyekuwa chifu
wa Kasulu aliyesimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga
mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru.“Bibi Titi Mohamedi ambaye alikuwa
kiongozi wa TANU- Women Wing aliweza kutengeneza historia ambayo sio rahisi
kufikiwa au kuvujwa na kiongozi wa vyama vya siasa katika mazingira ya sasa,” lakini
bado wamekuwa hawapewi kipaumbele kinachostahili
Ameongeza kuwa yupo pia Sophia
Mustapha (mwenye asili ya Ki- asia) ambaye pamoja na sera za kibaguzi,
zilizokuwa zimewekwa na wakoloni za kuwabagua raia kwa misingi ya rangi,
aliamua kuunga mkono juhudi za TANU na alishiriki siasa na hatimaye kuingia
katika baraza la kutunga sheria.
Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) Lilian Liundi , amesema
dhima ya kampeni hiyo ni “Uthubutu wa mwanamke na miaka 54 ya maendeleo ya
Tanzania” huku kaulimbiu ikiwa ni “Mwanamke, Historia yetu, fahari Yetu”.
Katika kampeni hiyo ambayo
imezinduliwa inatarajiwa kukusanya Taarifa zitakazotumika kuwaenzi wanawake kama sehemu
ya kuhamasisha vizazi vya sasa na vijanvyo umuhimu wa ushiriki wa wanawake
katika maendeleo endelevu.
“Kuendeleza mijadala kuhusu michango
na ushiriki wa wanawake na kudai uelekezaji wa rasilimali kutoka kwa wadau
mbalimbali katika kuendeleza ushiriki wanawake na kuwaenzi,” amesema Liundi.
Kampeni hiyo itachukua muda wa miaka
mitatu. Inatarajiwa kuhusisha wadau mbalimbali wakiwemo TGNP Mtandao,
Makumbusho ya Taifa, Women Research Development Project, Women Fund Tanzania
(WFT), Soma na shule ya uandishi wa habari ya RAIDA
Kwa mujibu wa wadau ambao wamefika
katika sherehe za uzinduzi huo wamekiri na kusema kuwa mradi huo ni muhimu sana
katika kufanya vizazi vyetu kujua mashujaa ambao wamefanya kazi kubwa katika
taifa hili la Tanzania.


No comments
Post a Comment