HABARI KUBWA ,TAARIFA KAMILI KUFUKUZWA KWA ZITTO KABWE,TUNDU LISSU AMMALIZA KABISA UBUNGE BY BY,MWENYE AUFYATA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu akizungumza mda huu na waandishi wa Habari ofisi kwake |
SAFARI ya
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ndani ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema ni wazi imefikia Mwisho,Baada Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam,kubariki
maazimio ya Kamati kuu ya Chadema yaliyomfukuza uanachama kwa madai ya usaliti,Anaandika
KAROLI VINSENT,endelea nayo.
Zitto Kabwe ambaye alifukuzwa Chadema
baada Kudaiwa kuandaa mipango ya siri ya kuupindua uongozi wa Juu wa chama hicho na
ukiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe,
Ambapo
yeye Zitto alikimbilia mahakama kuu kuzuia Kamati ya Chadema isimjadili .
Akitoa hukumu hiyo leo, Jaji wa Mahakama kuu ,Richard Mzirah amesema amekubalina na
maazimio yaliyofikiwa na Kamati kuu ya Chadema na kumtaka Mbunge huyo alipe
garama za kesi zote.
Akizungumzia Uamuzi huo wa Mahakama
kuu, mda huu Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar Es Salaam ,Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema Tundu Lissu wakati wa Mkutano na waandishi wa habari,ambapo
amesema anaipongeza Hukumu ya Jaji Mzirah na kusema imefuata taratibu za
sheria.
“Kwanza nasema sisi Chadema tumepokea
kwa furaha uamuzi wa Mahakama kuu chini ya Jaji Mzirah na tunasema kwanza
mahakama imefanya haki sana katika kutoa hukumu sahihi,kwasababu vyama hivi
vinaongozwa kwa taratibu na sheria zilizowekwa,na mtu ambaye aliaminika lakini akawa anafanya mipango ya
kuupindua uongozi wa chadema na chama kimechukua maamuzi sahihi”amesema Lissu.
pichani ya Dokta Slaa na Mwanashelia wa Chadema Piter Kibatala |
Tundu lissu ameongeza kuwa kwa sasa
Chama hicho hakimtambui Zitto Kabwe na kitaiandikia Barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC na wao
watamuandikia barua Katibu wa Bunge naye atampelekea Spika wa Bunge Anne Makinda kwamba
wamuondoe kwenye nafasi ya Ubunge.
“Kwasababu
kitendo chake Zitto kwenda makamani kuishitaki viongozi wa juu wa Chadema
Mahakamani ni teyari amejifukuzisha mwenyewe na katiba iko wazi sisi atumtambua
kama mbunge wetu ”Ameongeza Lissu.
Aidha,Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kwa sasa
anawataka wanachama wote wa Chadema kuwa watulivu katika kipindi hiki cha
Mpito.
Mtandao huu ulimtafuta Zitto Kabwe.
Mwandishi wa
Mtandao huu alipomtafuta Zitto hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuita na
kutopokelewa na badala yake alipotumia ujumbe mfupi,alijibu na kusema kwa sasa
yupo kwenye Vikao vya Kamati ya Bunge.
Maoni 1
Huyo mwanasheria pichani sio kibatala
Chapisha Maoni