Zinazobamba

HABARI KUBWA ,TAARIFA KAMILI KUFUKUZWA KWA ZITTO KABWE,TUNDU LISSU AMMALIZA KABISA UBUNGE BY BY,MWENYE AUFYATA SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu akizungumza mda huu na waandishi wa Habari ofisi kwake


SAFARI ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ni wazi imefikia Mwisho,Baada  Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam,kubariki maazimio ya Kamati kuu ya Chadema yaliyomfukuza uanachama kwa madai ya usaliti,Anaandika KAROLI VINSENT,endelea nayo.
      Zitto Kabwe ambaye alifukuzwa Chadema baada Kudaiwa  kuandaa mipango ya siri ya kuupindua uongozi wa Juu wa chama hicho na ukiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe,
     Ambapo yeye  Zitto alikimbilia mahakama kuu kuzuia Kamati ya Chadema isimjadili .
           Akitoa hukumu hiyo leo, Jaji wa Mahakama kuu ,Richard Mzirah amesema amekubalina na maazimio yaliyofikiwa na Kamati kuu ya Chadema na kumtaka Mbunge huyo alipe garama za kesi zote.
           Akizungumzia Uamuzi huo wa Mahakama kuu, mda huu Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar Es Salaam ,Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu wakati wa Mkutano na waandishi wa habari,ambapo amesema anaipongeza Hukumu ya Jaji Mzirah na kusema imefuata taratibu za sheria.
        “Kwanza nasema sisi Chadema tumepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama kuu chini ya Jaji Mzirah na tunasema kwanza mahakama imefanya haki sana katika kutoa hukumu sahihi,kwasababu vyama hivi vinaongozwa kwa taratibu na sheria zilizowekwa,na mtu ambaye  aliaminika lakini akawa anafanya mipango ya kuupindua uongozi wa chadema na chama kimechukua maamuzi sahihi”amesema Lissu.
pichani ya Dokta Slaa na Mwanashelia wa Chadema Piter Kibatala
        Tundu lissu ameongeza kuwa kwa sasa Chama hicho hakimtambui Zitto Kabwe na kitaiandikia Barua  Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC na wao watamuandikia barua Katibu wa Bunge naye atampelekea Spika wa Bunge Anne Makinda kwamba wamuondoe kwenye nafasi ya Ubunge.
“Kwasababu kitendo chake Zitto kwenda makamani kuishitaki viongozi wa juu wa Chadema Mahakamani ni teyari amejifukuzisha mwenyewe na katiba iko wazi sisi atumtambua kama mbunge wetu ”Ameongeza Lissu.
           Aidha,Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kwa sasa anawataka wanachama wote wa Chadema kuwa watulivu katika kipindi hiki cha Mpito.
  Mtandao huu ulimtafuta Zitto Kabwe.

Mwandishi wa Mtandao huu alipomtafuta Zitto hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuita na kutopokelewa na badala yake alipotumia ujumbe mfupi,alijibu na kusema kwa sasa yupo kwenye Vikao vya Kamati ya Bunge.

Maoni 1

Unknown alisema ...

Huyo mwanasheria pichani sio kibatala