HABARI KUBWA LEO-YAMEFICHUKA YA KOMBA,SIRI YA KIFO YAFICHUKA,WANAOMLILIA WANAFANYA UNAFIKI TU SOMA HAPA KUJUA
MBUNGE wa Mbinga Magharibi (CCM), John Komba,
amefariki dunia kutokana na kuzongwa na mzigo wa madeni, likiwamo mkopo kutoka
Benki ya CRDB.
Taarifa zinasema, benki
hiyo ilitoa kiasi cha sh. 12 bilioni kwa mwanasiasa huyo mwaka 2009, lakini
hadi mauti yanamkuta, alikuwa hajaweza kulipa deni hilo. Anaripoti
Saed Kubenea…(endelea).
Habari zinasema, wakati Komba akihaha
kuokoa nyumba yake kutokana na tanganzo la benki ya CRDB kwenye vyombo vya
habari; huku akiwa tayari ameonekana kukata tamaa; ghafla Jumamosi jioni
alipatwa na shinikizo la damu na kufariki dunia.
Mamilioni hayo ya
shilingi yalitolewa na CRD Benki kwa mbunge huyo kwa ajili ajili ya kuendeleza
shule zake mbili alizokuwa akizimiliki – shule ya Sekondari ya Bakili Muluzi na
Shule ya Msingi ya Coletha – zilizoko jijini Dar es Salaam.
Hadi anafariki dunia,
Komba alikuwa amebakiza kiasi cha zaidi ya sh. 78.5 milioni. Deni la Benki
linatokana na mkopo pamoja na riba ya asilimia 17 katika kipindi cha miaka
mitano ya uhai wa mkopo.
Komba amefariki
dunia Jumamosi iliyopita, miezi mitatu baada ya Benki ya CRDB kuuza shule zake.
Mbali na kuuza shule,
benki iliuza vifaa mbalimbali, likiwamo eneo la ukubwa wa mita za mraba zaidi
ya 34,000 lililotumika kutoa mkopo wa sh. 900 milioni mwaka 2009.
Shule za Komba pamoja
na vifaa vyake, vimenunuliwa na mfanyabiashara mmoja mmoja.
Chanzo chetu kilimeelezwa
kuwa Komba alijaribu, bila mafanikio, kushawishi serikali kununua shule yake;
na kwamba alitinga hadi ikulu na makao makuu ya CCM kuomba msaada ili shule na
nyumba yake visiuzwe.
Hata hivyo, taarifa zinasema, Komba hakufanikiwa kupata msaada wa
kuzuia shule kuuzwa. Hadi anafariki dunia benki ilikuwa inajiandaa kuuza nyumba
yake.
“Yule bwana alifika
hadi ikulu kuomba msaada ili nyumba yake isiuzwe. Alitaka serikali imsaidie
kununua shule yake; au kuomba benki izuie kwa muda uuzaji kwa kuwa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilikuwa limekubali kununua eneo hilo kwa
bei ya soko,” ameeleza mtoa taarifa.
Baada ya shule
kuuzwa na deni kushindwa kumalizika, mtoa taarifa anasema, Komba alirudi tena
ikulu na CCM kuomba msaada wa kukwamua nyumba yake.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, alijaribu kunusuru shule ya Komba kupigwa mnada kwa kuiandikia
benki ya CRDB kumpa mwanasiasa huyo muda zaidi wa nyongeza ili kulipa deni lake.
Hata hivyo, pamoja
na maombi ya Pinda kupewa nafasi, bado Komba alishindwa kulipa deni hilo.
Komba aliyekuwa anajulikana kwa jina maarufu la “Mzee wa kutoa
mitaji kwa vimwana,” alizikwa juzi Jumanne, katika jimbo lake la uchaguzi la
Mbinga Magharibi.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni