UFISADI WA ESCROW, ZITTO KABWE AWEWESEKA,SASA ACHUTAMA NA KUIANGUKIA TUME YA MAADILI SOMA HAPA KUJUA
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Kabwe Zitto, ameombwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Mbunge
wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), zichunguzwe. Anaandika
Mwandishi wetu…(endelea).
“Naiomba Sekretariati ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya
Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi.
Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi,” amesema.
Hatua hiyo inakuja
baada ya Ngeleja kumtaja Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), kuwa amepokea mgawa wa fedha za kutoka akaunti ya Escrow sh. milioni
30 lakini Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
halijamwita kumhoji.
Katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari, Zitto amesema katika kujitetea mbele ya Baraza la
Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya
Escrow, Ngeleja amesema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na
wafanyabiashara na taasisi za umma.
“Katika maelezo yake
alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba
nilipewa fedha na kampuni ya PAP na nilipewa fedha na shirika la NSSF.
“Tuhuma zote hizo
nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na
zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa
malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo,” amesema Zitto.
Kwa mujibu wa Zitto,
watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya
kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na
kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao.
Zitto ameongeza kuwa
ndio maana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba
huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.
“Hivyo, narudia
kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja,
wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza
la Maadili kujieleza.
“Nikiwa mbunge
ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea
mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi
zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma
zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu,”
ametamba Zitto.
Mbunge huyo ameungwa mkono
kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Kwamba ni kazi ambayo
ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo
viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya
mafuta mazito kuendesha mitambo ya umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za
umma bila kulipa, kujilimbikizia mali tofauti na kipato.
“Naiomba Sekretariati
ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu
wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi,”
amesema.
Zitto ameongeza kuwa
katika kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi
aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili.
Amesema kuwa Baraza
likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa
imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi Online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni