EXLUSIVE-GAZETI LA MBOWE LAMALIZWA TENA,CHAMA CHA ACT YAIBOMOA GAZETI LAKE SOMA HAPA KUJUA
KAMA ni Majanga basi ndio yanayolikuta gazeti
la Tanzania Daima ambalo
linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema,Freeman Mbowe,baada ya hivi sasa kukimbia na lundo la wahariri na waandishi wake
wa Habari, ambapo sasa mwandishi wake muhimu Abdallah Khamis amehama rasmi
gazeti hilo linalotoka kila
siku.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Taarifa za kuamika ambazo mtandao huu
umezipata zinasema kwa sasa ni wazi gazeti hilo limekuwa likipungukiwa waandishi wake baada
ya Mwandishi muhimu Abdalla Khamis kulitema gazeti hilo na kwenda kwenye chama
kipya cha siasa cha ACT-Tanzania na kuukwaa nafasi ya Afisa Habari wa chama
hicho.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu
aliyoko ndani ya Gazeti la Tanzania Daima anasema kwa sasa gazeti limekuwa
likipitia katika kipindi kigumu,ambapo anadai kuondoka kwa Abdallah Khamis
ni wazi sasa gazeti hilo linaingia kwenye kipindi kigumu.
Pichani ni Abdallah Khamis |
“Yule bwana Khamis ni mwandishi mmoja
ni mzuli sana tena mimi kama mwandishi mwenzake
nasikitika sana kwa uongozi kumwacha mwandishi huyo aondoke kirahisi
hivyo,maana ukizungumzia Abdalla unazungumia kiungo muhimu sana na sijui hatma
ya gazeti baada ya kuhama yeye”ametupasha mtoa huyo taarifa.
Mtandao huu umenasa barua ambayo
imethibitisha ni wazi amekuwa Afisa Habari wa ACT-Tanzania,kwa mujibu wa Barua
hiyo ambayo yeye Abdallah alikwa akiwataarifu waandishi mbalimbali wa
vyombo vya Habari kwamba chama cha ACT-Tanzania[FPM1] kitakuwa na Mkutano mkuu ambao unaotarajia
kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Ambapo barua
hiyo inasomeka hivi
“Chama cha
ACT-Tanzania kitafanya Mkutano wa Halmashauri Kuu,Kamati kuu na Uzinduzi wa
Chama kuanzia machi 27-29/2015 Kutokana na umuhimu wa chombo chako katika
kuupatia umma wa Tanzania habari sahihi, tunakaribisha uwakilishi kutoka kwako
katika shughuli hiyo. Tunaomba mtupatie majina ya waandishi na wapiga picha
watakaohudhuria matukio hayo kwa siku hizo tatu. Asante kwa ushirikiano wako
Abdallah Khamis Afisa Habari”.
Nafasi hiyo ya Afisa habari wa chama
hicho ilikuwa ikishikiliwa hapo awali na Karama Kaira,ambaye haijasemekana mara
moja amepewa nafasi gani ndani ya chama hicho kichanga cha siasa nchini.
Kuhama huko kwa Mwandishi huyo kunazidi
kuliacha gazeti la Tanzania Daima katika wakati mgumu ambapo wiki chache
zilizopita Gazeti hilo liliondokewa na Mhariri wake muhimu Edson Kamukara
ambaye ametimkia gazeti la Mawio,
Mbali na Kamukara wahariri wengine
waliolikacha Gazeti hilo ni Amana Nyembo ambaye nae ametimkia Gazeti la
Mwananchi na kuwa sub editor.
Mhariri mwengine aliondoka Gazeti hilo
aliyekuwa Mhariri Mtendaji Ansbert
Ngurumo ambayo naye ametangaza kuachana na gazeti hilo ambapo inasemekana
anajiaadaa kugombania Ubunge hapo kwenye uchaguzi mkuu hapo baadae kwenye mikoa
ya kanda ya ziwa na Nafasi yake kujazwa na kwenye Gazeti hilo ikajazwa na Neville Meena,ambaye alikuwa Mwandishi wa Gazeti la
Mwananchi
Waandishi waliohama.
Achia mbali
Wahariri,kuna waandishi mbalimbali waliohama hivi karibu ni Shaban Matutu
ambaye amehamia Gazeti la Mtanzania na Lucy ngowi aliyehama hivi karibuni.
Wengine waliohama ni
Bwana Maziku aliyehamia kwenye Kampuni inayohusika na kusimamia magari ya Uda
na kuwa afisa habari.
Maoni 3
kuhama kwa waandishi na wahariri i jambo la kawaida sana
Sasa hapo pigo liko wapi acheni propaganda zenuu hapaa
Mweee? mbona habari haina kichwa wala miguu? ama ulikuwa unataka kutangaza huo mkutano a ACT kiujanja kwa kupitia njia ya kuama mwandishi?. Jamani wewe unamiliki blog, hivto chunga sana kuandika habari ambazo hazibebi kichwa na masikio bali zile zinazobeba akili na maarifa. SAWA SAWA.!! SUALA LA KUHAMA NI LA KAWAIDA HAKUNA MTU ANAYEKAA MILELE HASA KENYWE HII TASNIA YA HABARI. Mbona mimi nimehama Tanzania Daima? na nilikuwa nalo tokea 2007 hadi 2015, mwanzoni? nimeama na kwenda kwenye blog. Mtu anahama kwa mapendekezo yake na wala kuondolka si pigo kwani wapo na walikuapo zaidi yake..
Chapisha Maoni