HABARI KUBWA LEO-YALIYOMKUTA DK ULIMBOKA YAMKUTA KIONGOZI WA MAFUNZO YA JKT,USALAMA WA TAIFA WATAJWA SOMA HAPA KUJUA
GEOGE Mgoba, kongozi wa vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), waliokuwa wakishinikiza serikali ya kutekeleza ahadi yao ya kupatia
ajira ametekwa.
Taarifa
zinasema, Geoge ametekwa na wanaodaiwa kuwa watu kutoka Idara ya Usalama wa
Taifa (TISS).
Mgomba ni miongoni mwa vijana
waliokutana na viongozi wa juu wa serikali, akiwemo Balozi Ombeni Sefue.
Serikali iliahidi ulimwengu
kuwa vijana wote watakaomaliza JKT watapa ajira. Ahadi hiyo haijatekelezwa.
Kutekwa kwa George kumefanywa kwa malengo mawili: Kwanza,
kumshawishi alegeze msimamo wa kuwaunganisha wenzake wanaoshinikiza serikali
kutekeleza ahadi yake hiyo mara moja.
“Lakini ikiwa hilo litashindikana, basi mpango umeandaliwa wa
kummaliza katika staili ileile iliyofanywa kwa Dk. Steven Ulimboka,” anaeleza
mmoja wa viongozi walioko katika mradi huo.
Kwa mujibu wa mtandao wa MwanaHALISI Forum,
Geoger ametekwa ili kutimiza mpango wa serikali wa kuzuia wimbi la vijana
waliomaliza mafunzo ya JKT, kuisumbua serikali.
“Tunawafahamu waliomteka Geoger. Nitawaumbua muda si mrefu,
humuhumu MF,” anaeleza mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online.
Anasema aliyemteka Geoger, siyo Ramadhan Ighondo ambaye alitajwa
katika sakata la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.
“Hawa ni tofauti,” anasema na kuongeza, “Ninamjua na tutawaumbua
muda si mrefu.
Chanzo ni Gazeti la Mwanahalisi.oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni