HABARI KUBWA LEO--CHENGE AIBANA MAHAKAMA MBAVU,ATEMA CHECHE ZAKE ZA SHERIA,NI SAKATA LA ESROW,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi , Andrew Chenge akitoka kwenye Kamati ya Maadili leo Jiji Dar Es Salaa |
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Magharibi,Andrew Chenge amesema anataka muongozo wa kujadiliwa yeye katika Tume ya Maadili kutokana na suala la Akaunti ya Tegeta Escrow liko Mahakamani hivyo shitaka lake haliko msingi wa kisheria ,Anaripoti KAROLI VINSENT ,Endelea nayo ..
Kugoma kwa chenge kwa shitaka lake kutosikilizwa na kutaka Tume ya Maadili itolee ufafanuzi juu ya kuwepo kwa Shauri kwenye Makama kuu ya Tanzania
linalozuia kujadiliwa kesi nje ya Mahakama hivyo kuhusu sakata la Akaunt ya
Tegeta Escrow kumetokea mda huu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anasomewa mashtaka yake kwenye tume hiyo ambapo---..
Chenge ambaye ni
Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali anashatakiwa na tume ya maadili kutokana na kitendo
chake che kupokea pesa ya zaidi Bilioni 1.6.8 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni
ya VIP Engineering bwana James Rugimalira wakati akiwa mtumisha wa umma na bila
kuitangaza kama zinavyodai sheria za tume hiyo.
Mbunge huyo
alipandishwa Mahakama ya Baraza la maadili mda huu Jijini Dar es Salaam mbele
ya Mwenyekiti wa Baraza hilo maadili Jaji Mstaafu Hamis Msumi -
Ambapo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Baraza Maadili Hassan Mayunga alidaiwa Mbunge huyo wakati akiwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2006 alivunja sheria ya maadili ya viongozi wa
umma kwa kuipa mkataba wa Miaka 20 kampuni ya kufua Umeme ya IPTL.
Wakili huyo amesema
kitendo iko cha Chenge kuipa mkataba kampuni hiyo kinaonekana wazi alikuwa
anamaslahi yake binafsi kwenye kampuni hiyo
na kupelekea kuingiziwa pesa na Mbia wa Kampuni ya IPTL ambayo ni VIP Engineering
na kupata mgao wa bilioni 1.6.8 kama zawadi ya kuingizia hasara serikali kwenye
mataba hao.
Mbunge Chenge akimgomea mwandishi wa habari wa Itv na Radio One Ufoo asimuulize swali lolote |
Mabishano ya Sheria yatokea
Mara baada
ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili huyo wa Baraza hilo ndipo Chenge akaliomba
Baraza hilo lisijadili kesi hiyo kutokana na kuwepo kwa kesi mahakama kuu
linalokataza Vyombo vyovyote vya Serikali visijadili suala linalohusu Mihamala
ya Akaunt ya Tegeta Escrow mpaka pale hukumu itakapotolewa.
Baada ya
kusema hivyo Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Hamis Msumi
Alimtaka Wakili
wa Baraza hilo kuhakiki hati ya Staka ya mahakama kuu na Wakili huyo akajitetea
na kusema hakuna kipengere kwenye kesi hiyo iliyoko mahakama kuu kinachozuia
vyombo vingine kuzungumzia.
Baada ya kusema hivyo Jaji Hamis Msumi h
akahahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili apate mda wa kusoma hati hiyo ya
mahakama kuu kama kutakuwa na kipengele hicho kwenye kesi na endapo kitakuwepo
basi Tume hiyo haiwezi kulizungumzia suala hilo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni