EXLUSIVE-GAZETI LA MBOWE LABOMOREWA,MHARIRI WAKE ATIMKA,KUBENEA ACHEKELEA SOMA HAPA KUJUA
PIGO
limelikumba Gazeti la Tanzania Daima baada ya Mhariri wake muhimu Edsoni Kamukara kuhama Rasmi Gazeti hilo
Anaripoti KAROLI VINSENT Endelea nayo
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao
huu umezipata zinasema Mhariri huyo ametimkia kwenye Gazeti linalotoka mara
moja kwa wiki Gazeti la Mawio.
Pichani ni Edsoni Kamukara |
“ni kweli Kamukara amehama kwenye
Gazeti letu na ametuga jana kwenye kikao,na hata sisi tumesikitika sana
kuondoka kwake maana ni mtu muhumi sasa,ukizungumzia watu muhimu sana walioleta
mafanikio gazeti letu lazima umtaje kamukara na sijui kwanini kaondoka maana
itatuletea pengo kubwa sana”kimesema chanzo chetu.
Kutimkia huko kwa Mhariri Kamukara
kunakuja wiki chache baada ya aliyekuwa mhariri mtandaji wa Gazeti hilo Ansbert
Ngurumo kuondoka na kutokana na y eye
kujiingiza kwenye masuala ya siasa,nafasi yake kuchukuliwa na Neville Meena.
Mbali na
Ngurumo wahariri wengine waliohama ni Amana Nyembo ambaye alikuwa mhariri wa
Makala naye pia ametimkia Gazeti la mwananchi na kuwa Mhariri pia yaani
(Sub-editor).
Wadau wahabari wanena.
Wadau
mbalimbali wa masuala ya habari waliozungumza na mtandao huu wameonyesha
masikitiko yao makubwa, baada ya kuondoka huko kwa mhariri huyo na kusema ni
pengo kubwa kwenye gazeti hilo bora linalotoka kila siku.
“Mchango wa kamukara ni kubwa sana katika
gazeti hili,leo hata mimi mwenyewe nilikuwa nafurahi sana kusoma makala zake na
hata Gazeti la Jumatano ambalo yeye analihariri, yaani utagundua huyo mtu anakitu
kimoja tofauti sana na wahariri wengine hapa nchini”alisema msomi mmoja wa
Shahada ya Habari kutoka chuo KIkuu cha Mlimani
Kwa upande
kiongozi mwengine kutoka ndani ya Idara ya Habari Maelezo ambaye akutaka jina
lake litajwe mtandaoni alisema Gazeti hilo litakuwa na changamoto kubwa sana
kwa utendaji wa Mhariri wake Mtendaji wa sasa,
Kuhamia huko kwa kamukara kwenye Gazeti
la Mawio ambalo linamilikiwa na Aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanahalisi, Lilofungiwa na
Serikali kwa mda usiojulikana Saed Kubenea na kushirikiana na Mkurugenzi mmoja
wa Fedha kutoka ndani ya Chadema jina tunalihifadhi ,kunatajwa ni njia ya
kulifanya gazeti la Mawio kuzidi kuwa juu.
Gazeti la Mawio ni miongozi mwa
magazeti yanayofanya vizunri sokoni,kwa mujibu wa utafiti uliofanya na mtandao
wa HABARI24.blogs,umelitaja gazeti hilo kuwa ni gazeti linalouza nakala myingi
kwa upande wa magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni