HABARI ILIYOTIKA JIJI-SAKATA UTEKAJI WA MJESHI,KAMANDA KOVA ARUKA KIHUNZI,MZIMU WA DK ULIMBOKA WAMTESA TENA SOMA HAPA KUJUA
Kauli hiyo ya Jeshi hilo la Polisi imekuja
huku bado Mwenyekiti huyo Bwana GEORGE S/O GALUS MGOBA, Miaka 28 akiwa amelezwa kwenye Hospitali ya
Muhimbili Jijini Dar es Salaam baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na
kutupwa kwenye Msitu ulioko Pugu Mkoa wa Pwani huku mwili huo ukiwa umechoka
kutokana na kipigo alichopigwa watekaji hao.
Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi
imetolewa mda huu Jijini Dar es Salaam,na Kamishna wa kanda Maalumm ya Dar es
Salaam Suleimani Kova wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kova huku
akisema kwa kujihamini amesema jeshi hilo haliamini kama kiongozi huyo ametekwa
mpaka pale watakapofanya uchunguzi na kulidhisha.
“Taarifa za kutekwa siwezi kuziaamini
mpaka tuunde tume ichunguze na tufahamu nani kamteka huyo mtu,ili tujue harafu
tuweze kubaini maana isije kuwa watu wanataka umahaarufu kwa kutumia mipango hiyo,na
tukimaliza kuchunguza kama ni kweli ametekwa tutachukua hatu”
“Kwasababu huyo mwenyekiti anasema
ametekwa na amechomwa sindano ya sumu na watekaji,kwanini sasa anakataa kupimwa
na madaktari,kuna nini hapa tena anataka hadi kutoroka hospitalini na juzi
tulimkamata nje ya mrango wa hospitali akitaka kukimbia sasa hapa kuna nin
jamani kwahiyo lazima tufanye uchunguzi suala hili”amesema Kamishna Kova.
Mtifuano wa Kamishan Kova na Waandishi
wa Habari
Katika hali ya
kushangaza wakati wa mkutano huo na waandishi Wa Habari ulibadilika na kuwa
sehemu ya Mabishano pale Waandishi hao walipokuwa wanataka ufafanuzi kuhusu
kurudia mara kwa mara kwa matukio hayo ya utekaji kwa watu mbalimbali kwaanzia—
Aliyekuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari nchini Dokta Steven Ulimboka na Mhariri Mtendaji wa
Magazeti ya NewHabari nchini Bwana Kibanda na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Mawio Saed Kubenea ambao wate walifanyiwa vitendo viovu na vya kihalamia.
Kamishna huyo akageuka mbogo na kuwataka Waandishi wa Habari waache maswali
ya Uchochezi kwani matukio hayo yalishafanyiwa kazi na ufumbuzi ulishapatikana
na aliwataka waandishi wakitaka kuuliza maswali ya hayo waandae siku maalum kwa
ajiri ya maswali na yeye atakuwa tayari
kuwajibu.
Katika hatua Nyingine
Jeshi hilo Kanda maalum ya Dar es Salaam limesema limewakamata vijana wapatao watano ambao ni viongozi wa “Umoja wa Kikundi cha wahitimu wa
mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa” kwa makosa ya uchochezi na mikusanyiko isiyo
halali jijini Dar Es Salaam. Watu hao wanatabia ya kujikusanya kwenye kundi la
vijana wasiopungua 300.
Kamishna Kova amesema Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa umoja huo hauna usajili kisheria na hakuna ahadi
yeyote ambayo kikundi hicho kimepewa.
Ambapo Kamishna huyo
amewataja Wanaohojiwa mpaka sasa ni pamoja na Mwenyekiti
wa kikundi hicho aitwaye GEORGE S/O GALUS MGOBA, Miaka 28, Mkazi wa Mabibo
Loyola.
Mwingine ni Katibu wa
kikundi hicho aitwaye LINUS S/O EMMANUEL, Miaka 28, Mkazi wa Tabata.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa umoja wa vijana
waliohitimu JKT anayejulikana kwa jina la PARALI S/O ARUWERA KIWANGO, Miaka 25,
Mkazi wa Temeke Mikoroshini, anatakiwa kujisalimisha haraka katika ofisi ya
Mkuu wa Upelelezi Polisi Kanda Maalum Dar es salaam au kituo chochote cha
Polisi cha karibu na mahali aliko. Mtuhumiwa huyo alitoroka baada ya kugundua
katibu wake amekamatwa hivyo anatakiwa ajisalimishe kuhojiwa kwa matukio hayo.
Kamishna huyo amesema Katika
suala hili la wahitimu wa JKT, kuanzia sasa Jeshi la Polisi litachukua hatua
kali kudhibiti mkusanyiko au mkutano wa aina yeyote kwani haina uhalali wowote
kisheria. Imegundulika kwamba mikusanyiko ya vijana hawa ni uchochezi na siyo
halali kisheria hivyo haikubaliki. Yeyote atakayejaribu kushiriki katika
mkusanyiko wa aina hiyo awe ni kiongozi au mjumbe atachukuliwa hatua kali
haraka sana.
Historia ya kutekwa
Mnamo tarehe 22/02/2015 majira ya saa 11:45 jioni mtuhumiwa GEORGE S/O
GALUS akiwa chini ya ulinzi alijaribu kutoroka kutoka wodini katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa lakini Polisi walimbaini na kumkamata kabla
hajatokomea. Jalada la utoro chini ya ulinzi halali limefunguliwa na uchunguzi
linaendelea.
Aidha tukio la mtuhumiwa
GEORGE S/O GALUS kudai kutekwa kati ya tarehe 16/02/2015 hadi 19/02/2015
linaendelea kuchunguzwa kwa ushirikiano kati ya Mkoa wa Pwani na Polisi Kanda
Maalum ya Dar es salaam ili kubaini ukweli wa taarifa hiyo na kuwajua
wanaosemekana kumteka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni