FREEMAN MBOWE ALIPUKA,NI KUHUSU UCHAGUZI 2015,ASEMA NENO KALI SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Freeman Mbowe picha na Maktaba |
Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimejipanga kuhakikisha katika
uchaguzi Mkuu hawaibiwi kura.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freemon Mbowe wakati
akizindua mafunzo ya Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha chama hicho (Red
Brigade), kwa vijana 200 wa Kanda ya Kati pamoja na Kikosi maalum cha
Karate.
“Katika
uchaguzi huu hatutaki kulalamika tena kwamba tumeibiwa kura na
tutahakikisha tutaomba kura kwa wananchi na tutazilinda,” alisema
Mbowe.
Alisema endapo
watakubali kuibiwa kura maana yake hawapo tayari kuongoza.
Mbowe aliwataka
vijana hao wa Brigade kutokukilinda chama peke yake bali pia kiwe chachu
ya ulinzi kwa jamii inayowazunguka kwenye maeneo yao.
Alibainisha
kuwa Chadema kitaendelea kutoa mafunzo ya ulinzi kwa vijana nchi nzima.
"Vijana
hawa lazima wajenge moyo wa kujitolea, chama kilijengwa na watu wenye moyo
huo ambao baadhi walipata madhara mbalimbali ikiwamo kupoteza maisha,” alisema
Mbowe.
Alisema wajenge sifa ya kuwa
wakombozi wa Taifa na malipo mengine siyo lazima walipwe hapa duniani
bali watapata kwa Mungu.
Taarifa
muhimu kuhusu chadema nyingine soma hapoa chini
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kutumia mabaraza yake kufanya
mashambulizi ya kisiasa kujiimarisha miongoni mwa makundi maalum katika jamii.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho,
chama hicho sasa kitayatumia mabaraza yake ya Vijana (Bavicha), Wanawake
(Bawacha) na (Bazecha) kama mkakati wa kulenga makundi mahsusi ya wapiga kura
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Habari hizo zilisema kuwa chama hicho kiliyaagiza mabaraza hayo
tangu mwaka jana kuhakikisha yanahamasisha makundi maalum katika jamii na
kuwa mstari wa mbele kwenye mapambano ya kisiasa ya chama hicho.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini
Makene, alipoulizwa juu ya taarifa hizo, hakukubali ama kukanusha.
Makene alisema anachofahamu viongozi wakuu wa chama hicho
wametawanyika sehemu mbalimbali nchini kwenye shughuli za kukijenga chama.
“Kama unavyojua, hatujawahi kupumzika tangu uchaguzi mkuu wa
mwaka 2010, tumekuwa tukibadili gia na kuongeza umakini kadiri ya matakwa ya
safari ya kisiasa ambayo inazidi kushuhudia Chadema na upinzani kwa ujumla
ikizidi kuungwa mkono huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), nacho kikijaribu
kupambana na sisi kwa kutafuta mlango wa kutokea,” alisema Makene na kuongeza:
“Lengo la viongozi hao wakuu kutawanyika nchi nzima ni
maandalizi mahususi kwa ajili kuwapatia fursa viongozi hao kushughulika na
masuala makubwa ya kukiandaa chama ili kishinde na kushika dola kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.” Makene alisema mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alikuwa Shinyanga kufunga mafunzo
ya uzalendo na ukakamavu kwa vijana na kufanya mkutano wa hadhara Solwa pamoja
na kuendesha vikao vya kuimarisha mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni