Zinazobamba

HABARI MBAYA DAR LEO-MAGOROFA YAUNGUA,NI NHC,KAMANDA KOVA AONYESHA UMWAMBA WAKE SOMA HAPA KUJUA


Moja ya Jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya mtaa wa Libya na Mosque likiendelea kuwaka moto huku Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiangalia namna ya kuudhibiti moto huo.
Gari la Zimamoto la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam likiwasili eneo la tukio.
Kazi ikiendelea.
Mara mabomba kadhaa yakazidiwa na nguvu ya maji na kupasuka,lakini haikuwa tatizo kwani ilikuwe mingine kibao ya rizevu.
Kazi ikiendelea.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akijaribu kufanya mawasiliano na vyombo mbali mbali vya zimamoto.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio la Moto Mkubwa uliozuka mapema leo kwenye majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yaliopo kwenye makutano ya mtaa wa Libya na Mosque kuteketeza eneo lote la juu la Majengo hayo.Chanzo cha moto huo hakikuweza fahamika mpaka tunaingia mitamboni japo tetesi zinaeneleza kwamba ni hitilafu ya uemem.
Kazi zilisimama kwa watu wengine wa maeneo ya jirani na tukio hilo.
Vikosi vya Zimamoto toka makampuni mbali mbali vilijipanga vyema kabisa kukabiliana na tukio hilo.
Kikosi cha Zimamoto cha Faya kikiendeleza uhodari wake wa kuzima moto ulioenea kila pembe ya majengo hayo.




Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeswad Nkongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.
Mwanalibeneke Othman Michuzi (kushoto) akiwa katika mavazi maalum pamoja na Maafisa wa Kikosi Zimamoto wakati wa zoezi la uzimaji moto huo mchana wa leo jijini Dar.
Sasa tumemaliza kazi na shukrani za dhati kwa maafisa wa kikosi cha Zimamoto waliokuwa bega kwa bega na wanahabari kuhakikisha uzimaji wa moto huo unakwenda vema.
MOTO umezuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.

Moto huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Polisi Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema vikosi vya uokoaji na Zimamoto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.

‘’Vikosi vya zimamoto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima moto na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa sana’’amesema Kova.



        
Kova amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa ushirikiano ambavyo ni  Zimamoto za Uwanja wa Ndege,Zimamoto ya Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate,Night Support ,pamoja  na Kikosi cha Zimamoto ya Jiji.

           Amesema kuwa  chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa na uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.

          Naye Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo na wanaweza kuudhibiti.

            Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es salaam na kuteketeza  mali kadhaa. Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..

Hakuna maoni