BREEKING NEWS-SAMWEL SITTA AFANYA UMAFIA BANDARINI,AMTIMUA KIGOGO WA JUU,NI YULE ALIYEKUWA ANARINDWA NA MWAKYEMBE SOMA HAPA KUMJUA
Pichani Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Bandarini aliyesimamishwa kazi Maden Kipande |
HABARI
iliyotufika mda huu zinasema Waziri wa Uchukuzi Samwel Siita amemsimamisha kazi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Maden kipande kutokana na
matumizi mabaya ya ofisi yaliyopelekea hasara serikali ya mabilioni ya shilingi,.
Kusimishwa huko kwa Mkurugenzi Kipande
kunatokana na Jitahada kubwa kati ya Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo
mtandao huu kufichua ufisadi uliokuwa unafanywa na Mkurugenzi huyo bandarini
ikiwemo huu hapa ANAANDIKA. KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Kwa Mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka katika Mamlaka hiyo
ambayo ni kitovu cha Maendeleo ya Nchi yetu ambazo mwandishi wa mtandao huu
amezipata ,zinasema mkurugenzi huyo amekuwa akiwasimamisha wafanyakazi kinyume
na Taratibu na sheria.
Chanzo hicho kinasema mkurugenzi huyo,amekuwa akiwasimamisha watu tu pasipo
kuwa na kosa lolote kwa mfano mwishoni mwa mwezi uliopita ameanzisha Mpango wa
kumngoa Meneja wa Bandari ya Tanga,Hassani Kyomile eti akisema Meneja huyo
amekuwa akivujisha siri kwenye Gazeti moja la wiki akidai Mhariri wa Gazeti
hilo ni Mhaya ,na meneja huyo pia ni mhaya eti anavujisha siri kwenye Gazeti
hilo,ambapo kipande anaona kumfukuza meneja huyo kutarahisisha mipango yake ya
kifisadi pasipo kuvuja.
Pichani ni Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta picha na maktaba |
Chanzo hicho kilizidi kusema Kipande
amekuwa akijivunia kwa Wanyakazi wake kwamba anaweza kufanya lolote na hakuna
wakumzuia,ambapo amesimamisha watu kazi zaidi ya miaka miwili huku wakiwa wakipokea mishahara pamoja na
malupulupu huku wakiwa nyumbani bila hata ya kufanya kazi.
Chanzo hicho
kiliwataja wafanya kazi hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa Masoko TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa
anavujisha siri(madudu)za TPA kuhusu
kwenye vyombo vya Habari,licha
ya mkurugenzi kipande alishindwa kutokea wala kukanusha kwenye vyombo vya
Habari juu ya Ufisadi huo ,
Tuhuma,zinginene zinazozidi
kumkabili kipande kuhatarisha usalama wa
Bandarini kwa kutokuna na kutokuwepo na Kamera CCTV pamoja na mita za kupima mafuta
yanayoingia nchini kutokafanya kazi kwa miaka mitatu sasa.
Jambo
la kushangaza Mama huyo Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na
kipande,lakini hajahojiwa wala
kurudishwa kazini ,huku akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupumarupu
mengine bila kufanya kazi hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho kilizidi kutaja orodha ya Wafanyakazi walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi mwingine ndugu Msemo,aliyekuwa Afisa
Ununuzi,naye alisimamishwa kazi tangu agosti2013 kwa tuhuma zisizokuwa za
Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye anaendelea kuchukua mshahara pamoja na
marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa na kipande kwa tuhuma hewa
Hery Arika,aliyekuwa Men eja
Biashara wa Bandari ya Dar es Salaam,alihamishiwa makao makuu na kuambiwa
kuripoti idara ya utawala tangu April 2013 hadi leo hii,Analipwa mishahara na
marupurupu yake bila kufanya kazi kwa mwaka mmoja sasa,kwa madai ya Kipande
hamtaki.
Ajira za
Upendeleo,
Kama kuna mgogoro unaofuka Moshi
Ndani ya Bandari basi ni huu unaotokana na
Ajira za Mhandisi Alois Matei,ambaye ni Naibu Mkurugenzi mkuu(Maendeleo
ya Miundombinu)na mhandisi William Shilla,ambaye ni mkurugezni wa
Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa Wahandisi hawa wawili waliajiriwa na Kipande kupitia Mlango wa Nyuma ,pasipo
kufuata taratibu za sheria.
Huu ni Mwenderezo wa Unyama
unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa Hatua yeyote kutoka
kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara husika ya Uchukuzi
ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande akinijinadi kwenye
mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote atakaye pingana nae
anamngoa kwani yeye na mamlaka hiyo ya Bandari hawapati hasara yeyote bali
serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyeto atakaye pingana
naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru,
hizo zinasema mzee Kipande amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi huku
akijinadi Hakuna mtu wa kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo
mmoja aliyoko Ikuru ya Jakaya
Kikwete,ambae amekuwa karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya Vitendo
hivyo akijua hakuna mtu wakumchukulia Hatua zozote
Hakuna maoni
Chapisha Maoni