BAROZI SEIF IDD AFUNGUA MKUTANO WA KIKANDA WA UKUAJI WA MAISHA YA BAADAE KWA MIJI YA AFRIKA,JIJINI DAR LEO
Balozi Seif Ali Idd afungua mkutano wa kikanda wa Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,jijini Dar leo
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd
(wa pili kushoto) akiwa katika meza kuu pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi
ya Waziri Mkuu - TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam,Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia),Mtendaji Mkuu wa Taasisi
ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo (katikati) pamoja na Dkt. Remy
Sietchiping kutoka UN-Habitat wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili
Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye
Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. Picha na Emmanuel
Masaka,Globu ya Jamii.
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo akizungumza wakati wa
ufunguzi Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa
miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar
es salaam.
Muwakilishi
kutoka Shirika la UN-Habitat,Dkt. Remy Sietchiping akifafanua jambo juu
ya changamoto mbali mbali zinazoikabili miji mingi ya mikubwa Afrika
Mashariki wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya
baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt
Regency,Jijini Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo akiteta jambo na Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd
wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa
miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar
es salaam.Katikati ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia.
Sehemu
wa washiriki wakiw katika Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa
maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya
Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam.
Mtoa
Mada katika Mkutano huo,Prof. David Simon akizungumza jambo wakati
Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya
Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es
salaam.
Mmoja wa wadau wa Mkutano huo akichangia mada.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa
Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya
Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es
salaam.
Picha ya pamoja.
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd,amesema watu wegi waonaishi maeneo ya mijini katika Afrika na dunia nzima wanapata changamoto ambazo ni lazima ziainishwe katika kuweza kuzikabili.
Balozi Idd ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kikanda uliowakutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika Mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika na jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050,uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
‘’Maeneo ya mjini katika Afrika yana fursa lakini maeneo hayo yana changamoto kutokana na ukuaji wa uchumi pamoja na mwingiliano wa kijamii’’amesema Balozi Idd.
Amesema maeneo ya mijini na majiji ni vituo vya fursa za uchumi,Teknolojia na sehemu ya kubadilishana mawazo na uzoefu na kufanya watu wa vijijini kuvutika zaidi wakiwemo vijana kukombilia mjini kwa ajili ya urahisi wa kupatikana kwa fursa pamoja na huduma mbalimbali.
Balozi Idd amesema watu wanaokwenda katika majiji wanajifunza njia mpya za kuishi na kufikiria jinsi ya kuendesha maisha yao kutokana na kuwepo hali hiyo majiji yanapambana dhidi ya umasikini na kuweka mikakati bora ya kuendesha majiji hayo.
Aidha amesema kushindikana na uimara katika miji na majiji matokeo yake ni umasikini unaingia ,magonjwa na kuwepo hali hiyo inaleta maswali ambayo yanatakiwa kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kuyatatua.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu,Profesa Joseph Semboja amesema jukwaa hilo la leo ni kuangalia changamoto na fursa mbalimbali zinazoletwa na ukuaji wa miji ya ukanda wa Afrika Mashariki na jinsi ya viongozi wa Afrika wanavyoweza kukabiliana nazo kwa pamoja.
‘’Kuna changamoto na uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika na duniani kwa ujumla wanaoishi mijini na kusababisha msongamano na shinizo la nyumba ,ajira huduma za kijamii’’amesema Prof.Semboja
Hakuna maoni
Chapisha Maoni