Zinazobamba

WASAKA URAIS WENGI NI WAGONJWA,YALIYOWAKUTA ZAMBIA KUIKUTA TANZANIA,JUKATA LAAPA KUFA NAO,SOMA HAPA KUJUA


MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA (JUKATA) AKIFAFANUA JAMBO KUHUSUMAMBO MBALIMBALI WALIOJIFUNZA HUKO ZAMBIA KATIKA UCHAGUZI WA RAIS KUFUATIA KIFO CHA RAIS MICHAEL CHILUFYA SATA
 Unaweza kusema kama ni dongo kwa wasaka urais ambao wameonyesha nia ya kwenda ikulu ya magogoni ambapo sasa Jukwaa la katiba nchini JUKATA wamejitokeza na kuja na hoja ya kila anayetaka kuingia ikulu sasa hana buni kupimwa afya yake na taarifa ya vipimo vyake na lazima vitangazwe hadharani ili kila mtanzania apate fursa ya kujua ni nani yuko mzima na yupi ni mzigo ili waweze kufanya maamuzi sahihi,

Maamuzi ya kutaka wasaka urais kupima afya zao yamekuja kufuatia vifo mbalimbali katika taifa la Zambia kuonekana kuwa vimekuwa vya ghafla na hivyo kulighalimu taifa hilo ambalo hata uchumi wake ni wa kuungaunga kulazimika kuingia hasara za uchaguzi kutokana na kuondokewa viongozi wake katika hali ya uatata
 Akisoma taarifa yake mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo, mwenyekiti wa jukwaa la katiba Deus Kibamba, ambao walienda Zambia kushiriki kama waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi huo, JUKATA wamesema hali ambayo wameiona na kujifunza kutokana na uchaguzi huo ni kwamba taifa hilo la Zambia walifanya uchaguzi wao katika hali ya uwazi mkubwa lakini wamegundua kuwa ghalama za kufanya uchaguzi huo huwenda zisingeingiwa kama viongozi ambao wanawapeleka ikulu wangefahamu afya zao mapema,


Amesema sasa kuna ulazima wa kuangali upya sera yetu. ili watanzania enye nia ya kugombea ni lazima afya zao kwanza zifahamike, na kuongeza kuwa taasisi itakayoshughulikia kupima afya za wasaka urais ni lazima ziwe huru ili kukwepa madaktari kununuliwa na hivyo kutangaza matokeo ambayo si halali,

Tunajua mpaka sasa kunawagonjwa wengi wanaonekana wanataka urais kwa nguvu zote, sisi kama JUKATA tunaona ni vyema kwanza wasaka urais hao wajipime kuhusu afya zao kabla hawajaenda mbele na kuomba kura kwa watanzania tuwachague huku wakijua wazi kuwa wao ni wagonjwa.

Wito umetolewa kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa watu wote ambao wana nia ya kugombea nafasi nyeti katika serikali hususani nafasi ya urais hawana budi kupima afya zao na taarifa za afya zao ziwekwe hadharani ili kila mwananchi ajue kuhusu afya ya kiongozi anaetaka kumchagua,

 Mwenyekiti huyo amesema kwa uzoefu ambao wameupata toka chaguzi mbalimbali ambazo zimefanyika Africa,  zimeonyesha kuwa Viongozi wakubwa wamekuwa wakifa katika kifo cha kutatanisha, wengine wanakutwa wamekufa wakiwa wamelala, wengine ghafla tu mtu amekufa hivyo kuibua hoja ya kuwa na wasiwasi na viongozi ambao wanapewa madaraka kuwa afya zao haziko vizuri na wanakimbilia ikulu kwenda kupata matibabu ya bure toka kwa wananchi
Kama Tanzania tunataka kuwa na viongozi ambao afya zao hazitiliwi shaka basi ni vyema tukawa na mkakati wa kupima wawania urais tena katika hospitali ambayo kila mtu anaiamini na taarifa zao tupatiwe hadharani ili tuweze kujiridhisha kuwa tunachagua mtu ambaye ana afya njema hivyo kuondoa hasara ambazo huwenda taifa ingeingia kama tahadhaliza awali hazitachukuliwa,


Miongoni mwa viongozi ambao wanaonekana kuwania urais kwa mwaka huu ni Mbunge wa Monduli ambaye mwaka 2012 afya yake ilikuwa siyo nzuri ambapo moja ya gazeti maarufu hapa nchini liliandika habari kuhusu afya ya mzee huyo na kudai kuwa afya ya mzee huyo inaibua utata
Kama ulikuwa hujasoma habari hiyo ni hii hapa.
UTATA umegubika afya ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa baada ya taarifa mbalimbali kueleza kuwa yuko hospitalini nchini Ujerumani kwa matibabu.Takriban juma moja sasa kumekuwa na taarifa mbalimbali zikizungumzia afya ya Lowassa lakini hakukuwa na taarifa rasmi kutoka chanzo chochote kati ya Serikali, familia yake au Bunge kuzungumzia afya ya Mbunge huyo wa Monduli.

Jana, Lowassa akizungumza na mwandishi wetu kwa simu alisema kwamba yuko hospitali, bila kufafanua kuwa ni nje au ndani ya nchi, wala kueleza kinachomsibu.

Mahojiano hayo kati ya Lowassa na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Swali: Asalaam alaykum Mheshimiwa Lowassa.
Jibu: Waalaykum Salaam.

Swali: Mimi naitwa... (jina la mwandishi) kutoka gazeti la Mwananchi. Kwanza pole kwa matatizo ya kiafya yanayokusumbua.
Jibu: Ahsante.

Swali: Nimekupigia pamoja na kukupa pole, nilitaka kujua unaendeleaje na matibabu?
Jibu: Niko hospitalini kwa sasa naomba niache mambo mengine tutaongea baadaye.

Swali: Lakini, ni matibabu gani hasa unayopata?
Jibu: ... (akimtaja mwandishi) naomba niache niko hospitalini sasa hivi mambo mengine tuongee baadaye.

Lowassa alitoa majibu hayo majira ya saa nane mchana na alipopigiwa tena saa 10.20 jioni, alijibu kama ifuatavyo:

Swali: Naam, Mheshimiwa Lowassa nimekupigia tena mimi... (mwandishi akajitambulisha).
Jibu: ... Unataka nikuambie nini tena? Nilishakwambia niko hospitalini niache!

Swali: Sawa, natambua uko hospitalini, lakini wewe ni kiongozi ambaye umewahi kuwa Waziri Mkuu, hivyo Watanzania wangependa kujua maendeleo ya afya yako kutokana na utata ulioibuka na kama je, umelazwa hapo hospitalini au uko katika matibabu ya kawaida?
Jibu Niache, ninachokwambia niko hospitalini sasa unataka nini tena? Nisingependa kuzungumzia afya yangu kwa undani.

Bunge

Akizungumzia suala hilo juzi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema ofisi hiyo haijapata maombi rasmi ya mbunge huyo kwenda nje kwa ajili ya matibabu.

Dk Kashillilah alisema kwa utaratibu, Ofisi ya Bunge inashirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kuwapeleka wabunge wanaoumwa nje ya nchi baada ya kupata rufaa ambayo inatokana na ushauri wa kitaalamu wa madaktari wa ndani.

Alisema hadi juzi, hakuwa akijua aliko Lowassa na kama ana matatizo ya kiafya kama inavyozungumzwa au la: “Mimi ndiyo Ofisi ya Bunge na ndiyo nakwambia hatujapata maombi ya kutaka mheshimiwa Lowassa apelekwe nje ya nchi.”

Mtendaji huyo mkuu wa Bunge alisema wapo baadhi ya wabunge ambao huwa wanakwenda nje kwa vipindi maalumu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya baada ya matibabu lakini, katika orodha hiyo Lowassa hayumo.

“Tunao utaratibu wa baadhi ya waheshimiwa wabunge kwenda nje kwa mujibu wa ratiba zao kwa ajili ya kufanyiwa uangalizi wa kawaida wa afya zao. Lakini, hadi sasa (juzi) katika orodha hiyo mheshimiwa Lowassa hayumo,” alisema Dk Kashillilah.

Hata hivyo, kwa mujibu wa nafasi yake ya utumishi serikalini aliyokuwa nayo, Lowassa anaweza kupata matibabu nje ya nchi kwa kupitia utaratibu wa Serikali bila ya kuhusisha Bunge.

Juhudi za kupata Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda au Naibu wake, Dk Lucy Nkya zilishindikana kutokana na simu zao kufungwa na kutopatikana ofisini.
mwananchi
KUHUSU UCHAGUZI WA ZAMBIA
Kwamujibu wa taarifa ambayo tumepatiwa toka ofisi ya jukata kuhusu mwenendo wa uchaguzi huko Zambia, ofisi hiyo imesema kuna mambo kadhaa wamefanikiwa kujifunza nayo ni kama ifuatavyo na kwamba kama Tanzania tukitumia mambo hayo basi machafuko kwa hapa nchini ni historia,
  • Malengo makuu ya jukata huko zambia yalikuwa kwanza kabisa ni kutazama jinsi katiba inavyotumika na kutekeleza uchaguzi katika nchi husika na pili ni kujionea jinsi ya vyombo vya kikatiba vinavyofanya kazi yake wakati wa uchaguzi, katika malengo hayo jukwaa limebaini uwezo mkubwa wa utekelezaji wa katiba ambao hakika katika chaguzi zingine lazima ziige mfano huo, kifupi katiba iliheshimiwa.
  • Uchaguzi ulikuwa ni wa uhuru na haki, wao kama waangalizi wa kimataifa waligundua kuwa uchauzi katika nchi hiyo ulikuwa ni uwazi huku vyombo vya dola kama jeshi la polsi nalo likitekeleza wajibu wake bila kuumiza wananchi
  • Kuhusu jinsia, kibamba amesema bado tatizo si tu kwa Zambia bali hata kwa nchi za Africa zote, bado wameshindwa kuwaamini wanawake, lakini kwa Zambia kuna mwanamke mmoja toka FDD Bi EDITH NAWAKWI ameendelea kuonyesha ushindani japo bado siyo mkubwa.

Hakuna maoni